Pages

Thursday, February 27, 2014

UCHAGUZI BAGAMOYO KUFANYIKA APRILI 6, 2014

Tume ya Taifa ya imepokea barua kutoka kwa Mhe. Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuiarifu uwepo wa nafasi ya wazi ya Ubunge katika Jimbo la Chalinze lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Saidi Bwanamdogoaliyefariki dunia tarehe 22.1.2014. Baada ya taarifa hiyo, Tume imepanga ratiba ya uchaguzi mdogo katika jimbo la Chalinze kama ifuatavya;

1. Uteuzi wa Wagombea Ubunge utafanyika tarehe 12-Machi-2014
2. Kampeni za Uchaguzi zitaanza tarehe 13-Machi-2014 hadi 5-Aprili 2014
3. Siku ya kupiga kura ni jumapili tarehe 6-Aprili-2014


Wagombea wanatakiwa kuwasilisha fomu za uteuzi kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Chalinze siku ya uteuzi si zaidi ya saa 10:00 Alasiri. Tume inawaarifu wananchi wote pamoja na vyama vya siasa kufuata tariba iliyotolewa pamoja na kushiriki katika mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia siku ya uteuzi hadi siku ya kupiga kura ili watimize haki yao ya kikatiba ya kuvhagua viongozi wanaowataka.

Tume inawasisitiza wananchi wote katika maeneo husika kujitokeza kukagua  taarifa zao wakati wa kuweka wazi daftari la kudumu la wapiga kura ili kuona kama kuna marekebisho madogo yanahitajika kufanyika kuwawezesha kupiga kura bila malalamiko yoyote. Ikumbukwe kwamba hakutakuwa na uandikishaji mpya wa wapiga kura.

Imetolewa na 
Julius Mallaba
Mkurugenzi wa Uchaguzi

No comments:

Post a Comment