Umoja wa
Mataifa umesema kuwa karibu watu milioni 4 wanahitajia msaada wa chakula
nchini Sudan Kusini kutokana na mgogoro wa nchi hiyo.
Toby
Lanzer mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan
Kusini amesema dola bilioni 1.3 zinahitajika kwa ajili ya kushughulikia
mgogoro huo. Lanzer pia amesema, mapigano ya nchi hiyo pia yameathiri
uchumi na kwamba raia wengi wa Sudan Kusini wanaishi kwa wasiwasi.
Maelfu ya
watu wakiwemo wafanyakazi wa utoaji misaada na wagonjwa wamelazimika
kukimbia nchini humo kutokana na mapigano kati ya vikosi serikali na
waasi watiifu kwa makamu wa rais wa zamani Riek Machar.
Mapigano hayo yameripotiwa kuendelea ijapokuwa makubaliano ya usitishwaji mapigano yamefikiwa kati ya pande hizo mbili.
Chanzo: kiswahili.irib.ir
No comments:
Post a Comment