Pages

Wednesday, February 12, 2014

UNALIJUA KABILA LA WANYAKYUSA?HISTORIA YAO FUPI HII HAPA ISOME



Wanyakyusa (pia huitwa Wangonde au Wasochile) ni kabila la watu wanaoishi kwenye wilaya ya Rungwe katika sehemu za kusini za Mkoa wa Mbeya (Tanzania) kaskazini kwa Ziwa Nyasa.
Lugha yao, inayoendelea kutumika sana, ni Kinyakyusa.
Mara nyingi Wagonde upande wa kusini wa mto Songwe nchini Malawi huhesabiwa pamoja nao katika kundi lilelile.
Mwaka 1993 watu zaidi ya milioni walikuwa wanajumlishwa kwa jina hili, takriban 750,000 upande wa Tanzania na 300,000 upande wa Malawi.

Historia

Kihistoria watu wanaoitwa leo Wanyakyusa waliitwa Wakonde, ambao kati yao Wanyakyusa walikuwa ndio kabila kubwa. Wakati wa karne ya 20 "Wanyakyusa" limekuwa jina la kundi kwa jumla.
Hadi leo kanisa la Kilutheri la KKKT linatumia jina "dayosisi ya Konde" kwa eneo lake katika mkoa wa Mbeya.
Wakati Wajerumani walipofika sehemu za kaskazini kwa Ziwa Nyasa mwisho wa karne ya 19 hawakuona tofauti ya kimsingi kati ya watu wa Malawi kaskazini na wale wa sehemu za Rungwe wakawaita wote "Wakonde" kutokana na jina lililokuwa kawaida ziwani.

Mgawanyiko wa Wanyakyusa

Wanyakyusa toka zamani walijulikana kama watu wa Konde. Wengi walikuwa kaskazini kwa ziwa Nyasa, lakini katika harakati za maisha na mabadiliko ya mazingira wengi wao wakakimbilia Mbeya mjini na sehemu nyingine.
Pamoja na hayo, hasa Wanyakyusa wapo wa aina mbili nao ni Wanyakyusa wa Tukuyu na Wanyakyusa wa Kyela.

Sifa za Wanyakyusa wa Kyela

1. Wengi si wapole mtu afanyapo kosa
2. Wacha Mungu
3. Wanajua kupenda
4. Hawapendi dharau
5. Wanapenda kujulikana (hasa kama wamesoma hadi kupata digrii n.k.)
6. Wapiganaji sana kimaisha
7. Wana wivu katika masuala ya mapenzi
8. Wanapenda haki itendeke, hawapendi ubabaishaji
9. Ni watu shupavu sana kwenye kazi za kujitolea hasa za kijamii

Sifa za Wanyakyusa wa Tukuyu

1. Wapole
2. Wacha Mungu
3. Wanajua kupenda
4. Hawapendi dharau kabisa
5. Wanajituma kwenye kazi, hasa kilimo
6. Wana wivu sana
7. Wanapenda haki itendeke na hawapendi ubabaishaji
8. Ni watu jasiri na wasioogopa vitisho
9. Ni welevu

ITAENDELEAAA USIKOSEEEEEEEE

No comments:

Post a Comment