Msaidizi wa rubani wa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, Halimedhin Abera, ndiye aliyebainika kuteka moja ya ndege za shirika hilo hivi karibuni.
Inadaiwa kuwa rubani huyo aliiteka ndege kwa sababu ya kuwa na msongo wa mawazo, baada ya kufiwa na mjomba wake.
Abiria mmoja aliyenusurika katika ajali hiyo
anasema, Abera aliwaamuru abiria wote kukaa chini, huku akiwatishia
kuzima hewa ya Oksijeni.
Abera, ambaye amelifanyia kazi shirika hilo kwa
miaka mitano, inadaiwa alifunga mlango wa chumba cha rubani (cockpit)
na kubadilisha mwelekeo wa ndege. Awali ndege hiyo ilikuwa ikielekea
Italia, lakini akaamua kuipeleka Uswisi aliposema alikwenda kuomba
hifadhi. Msimuliaji huyu wa mkasa anasema baada ya kuiteka ndege
alifungua maski za hewa ya oksijeni na kutishia kuizima kama abiria
wasingetulia.
Anasimulia: “Nilifikiri labda kuna tatizo la
kiufundi au kwa bahati mbaya mtu amebonyeza sehemu, abiria tulibaki
tukitazamana kwa sura za kuulizana ndani ya ndege.”
Anasema baada ya muda mfupi, sauti nzito
ikizungumza kwa jazba ilisikika kutoka katika vipaza sauti vya ndege
ikisema: “Kaa chini, ninazima hewa ya oksijeni”.
Msimuliaji anasema rubani huyo alikaa kimya kwa
saa sita bila kuzungumza, huku abiria wakiwa hawajui wanaelekea wapi
wala mwisho wao utakuwa vipi.
Anaongeza kusema kuwa wakati hayo yanaendelea,
wahudumu wa ndege waliendelea kugawa vinywaji, huku wakiwatuliza abiria
na kuwahakikishia kuwa safari ilikuwa salama.
Hata hivyo, wahudumu hao waliwaambia kuwa, hawana mawasiliano na rubani huyo kwa kuwa ameyakata.
“Wahudumu walikuwa wanagawa vinywaji na kutoa
maneno ya faraja, hata hivyo kuna wengine walikuwa wakitokwa machozi
mbele yetu,” anasema msimuliaji.
Baada ya kusafiri saa sita kimyakimya, ghafla
ndege ilianza kuzunguka huku ikiegemea upande mmoja na baada ya muda
ilibadilisha upande wa bawa jingine.
Anasema: “Niliona mwisho wetu umefika kwani ndege
sasa inaanguka. Nikitazama nje niliona mwanga lakini baada ya dakika
mbili nikaona giza tena,” anasema na kuongeza:
No comments:
Post a Comment