Viongozi
10 wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar, jana
wameachiwa kwa dhamana baada ya Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar kupunguza
masharti ya dhamana kutoka fedha taslimu Sh25 milioni kila mshtakiwa
hadi kuwa dhamana ya maandishi kwa kiwango hicho. Uamuzi huo umetolewa
baada ya upande wa utetezi,kuiomba mahakama kupunguza masharti ya
dhamana kwa kuwa hawana uwezo kutoa fedha taslimu. Kesi hiyo itatajwa
tena Machi 27.
No comments:
Post a Comment