Wanaume
wanaoshukiwa kuwa wanachama wa al-Shabaab wakisikiliza kesi yao katika
mahakama ya mwanzo ya Shanzu katika magereza ya Shimo La Tewa tarehe 3
Februari, kufuatia uvamizi wa polisi katika msikiti wa Masjid Mussa huko
Mombasa.
Kamishina
wa Kaunti ya Mombasa Nelson Marwa ametishia kufunga misikiti miwili
katika jiji hilo-- Masjid Mussa na Masjid Sakina -- kufuatia mapigana
baina ya polisi na vijana wa Kiislamu wiki iliyopita.
"Misikiti
hiyo ilikuwa ikishukiwa siyo tu inafanya kazi kama sehemu ya kutoa
mafunzo lakini pia kama eneo la kuandikisha askari wapya wa magaidi wa
al-Shabaab, na njia pekee ya kuwashughulikia ni kuifunga," Marwa
aliiambia Sabahi, ingawaje hakubainisha tarehe rasmi ya kufungwa huko.
Viongozi
wa dini na wahamasishaji wamepinga mpango wa serikali, hata hivyo,
wametahadharisha kwamba kufungwa kwa misiskiti hiyo kunaweza kuongeza
kuwafanya vijana kuwa na siasa kali.
"Hizo ni
harakati zisizokubalika na zinaweza kuongeza hali hiyo kwa kuwaudhi
vijana zaidi na kuimarisha hisia miongoni mwao kwamba serikali iko
kinyume nao, hivyo kuwafanya kuwa na siasa kali zaiidi," mjumbe wa
kamati ya msikiti wa Jamia wa Nairobi Ibrahim Lethome aliiambia Sabahi.
Lethome
alisema kufungwa kwa misikiti kungeweza hasa kuongeza ukiukwaji wa uhuru
wa kusali na kunaweza kuonekana kama kutoa adhabu ya jumla kwa ujumla
kwa jamii yote ya Waislamu.
Mpango wa
serikali "utafanya Waislamu kuona vita vyote hivyo dhidi ya ugaidi kama
vinavyolenga isivyo haki Waislamu ambako kutazuia ushirikiano baina ya
jamii na serikali", alisema.
Kuepuka
msimamo mkali zaidi katika misikiti, Lethome alishauri serikali kutumia
upelelezi kubaini kabla matukio yoyote ya uhalifu au shughuli
zinazohusiana na ugaidi katika maeneo ya swala.
Viongozi wa Kikiristo na Waislamu waungana
Viongozi wa dini wa Kikiristo pia walipinga kufungwa kwa misikiti.
"Hizo ni
harakati za mfarakano ambazo zilishauriwa vibaya na zisizo na tija kwa
kuchochea hisia za kidini ambazo zitafanya hali hiyo kuwa ngumu
zaidi,"Askofu wa Angalikana wa Dayosisi ya Mombasa Julius Robert Katoi
Kalu aliiambia Sabahi.
Kalu
alitoa wito kwa serikali kushughulikia suala la ukosefu wa ajira na
umaskini katika eneo hilo, ambazo pia ni sababu zinazowasukuma vijana
kuingia kwenye siasa kali.
Askafu wa
jimbo la askofu mkuu Willybard Lagho alisema kwamba badala ya kufungwa
kwa misikiti, serikali, pamoja na viongozi wa dini ya Kiislamu,
wangeangalia namna ya kubadilisha udhibiti wa misikiti.
"Msikiti
wa Sakina na Mussa ina kamati zake zinazoongozwa na maulamaa ambao
mipango yao ni kuingiza ajenda za siasa kali," Lagho aliiambia Sabahi.
"Uamuzi wa busara ungeweza kuwa serikali kusaidia kamati hizi kutwaa
tena udhibiti wa misikiti hii kuliko kuifunga."
Alilaumu
matumizi ya nguvu ya polisi na namna walivyovamia msikiti wa Masjid
Mussa, kuingia ndani wakati wakiwa mamevaa viatu vyao, akisema illikuwa
kukosa heshima katika nyumba ya kuabudia.
"Mtazamo
wa serikali una makosa," Lagho alisema. "Kutumia nguvu nyingi wakati wa
kushughulikia matukio haya ya msimamo mkali kunakofanywa na polisi kama
tulivyoona wakati wa uvamizi wa Jumapili, wenyewe tu ni msimamo mkali.
Serikali inapaswa kuwa na mjadala na kuhusisha jamii, [ambako] tuna
uhakika kunaweza kubadilisha hali ilivyo."
Ili
kushughulikia msimamo mkali huko Mombasa na sehemu nyingine za nchi,
Lagho alitoa wito kwa jumuia ya Waislamu kutafuta wahubiri na wanazuoni
wenye msimamo wa kati ambao wanaweza kuhubiri kwa vijana katika misikiti
iliyoathirika.
Wito wa uchunguzi, mjadala na suluhisho la kudumu
Siku ya
Ijumaa (tarehe 7 Februari) kamati ya kazi inayoundwa na wanazuoni wa
Kiislamu tisa na viongozi wa siasa walipelekwa Mombasa katika ujumbe wa
kutafuta ukweli wa mambo ili "kujihusisha na viongozi na vijana katika
hatua za kushughulikia matatizo yaliyopo katika chanzo cha mgogoro",
alisema Seneta wa Mandera Billow Aden Kerrow, ambaye anawakilisha kamati
ya kisiasa ya Waislamu na ni mjumbe wa kamati.
"Siku ya
Alhamisi, waumini wa Kiislamu, viongozi wa kisiasa na wa umma kutoka
Nairobi na Mombasa walikutana katika Msikiti wa Jamia huko Nairobi ili
kujadili matukio ya kusikitisha na kujutia katika Msikiti wa Masjid
Mussa ambayo yalisababisha mauaji ya watu nane," aliiambia Sabahi.
Kerrow
alisema timu itakuwa Mombasa kwa siku tano kabla ya kurejea Nairobi
ambako mkutano wa viongozi utaitishwa ili kutangaza matarajio ya
baadaye.
"Kwa sasa
hatuwezi kukupa maelezo yoyote kuhusu tume ya kutafuta ukweli wa
mambo," alisema."Tuko katika hatua ya kujielimisha wenyewe na kile
kinachotokea [na] tumeanza hatua za haraka za ujumuishaji ili
kuwaunganisha waliotengana na kutoa uongozi muhimu kwa vijana na jamii
ya Waislamu kwa ujumla."
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Haki za Binadamu cha Waislamu
(MHRF) Al-Amin Kimathi alitoa wito wa uchunguzi huru katika sababu za
vurugu za wenye msimamo mkali na unyanyasaji wa polisi ambao
umesababisha vifo vya wahubiri na vijana wanaohisiwa kuwa wanachama wa
al-Shabaab.
Uanzishaji
wa tume ya uchunguzi utasaidia kufichua vyanzo vya vurugu za wenye
msimamo mkali na kupendekeza utatuzi wa kudumu, alisema.
"Wakati
tunazungumza leo kila mtu, akiwa mtendaji wa serikali au mtendaji wasio
wa serikali, ana makosa na anapaswa kulaumiwa kwa kinachoendelea,"
Kimanthi aliiambia Sabahi. "Ni katika kujitathmini tu kupitia tume huru
ya uchunguzi kwamba tunaweza kuliangalia suala hili kwa ujumla ili
kutupa msingi wa kweli wa uingiliaji."
"Kwa
hiyo, tunataka serikali itoe uchunguzi huru katika sababu za vurugu za
kutisha katika Masjid Mussa na maeneo mengine na kutumia hatua
zinazokubalika kiraia na kisheria za kutambua na kushughulikia dalili za
ukereketwa wenye vurugu kutoka eneo lolote, iwe kidini au isiyo na
uhusiano wa dini, watendaji wa serikali au wasio wa serikali," alisema.
Tume ya
uchunguzi inapaswa kuongozwa na mtu ambaye ni sawa na jaji wa Mahakama
Kuu na ina wajumbe ambao wana utaalamu wa kijamii, kisiasa, kiuchumi na
kidini.
Alisema MHRF
imedai kuachiwa mara moja kwa watoto ambao walikamatwa katika vurugu na
kukamatwa wakati wa uvamizi wa Masjid Mussa. Asasi pia ilitoa wito wa
kushtakiwa kwa polisi ambao wanaweza kuwa wamejihusisha katika kutumia
nguvu nyingi ambazo zilisababisha vifo na kuumia kwa watu wasio na
hatia.
"[Serikali
inapaswa] kuahidi na kufungua njia za mjadala na uhusishaji na wote
wanaohusika kuleta ukuaji wa hatari wa ukereketwa wenye vurugu katika
jamii," Kimanthi alisema.
Chanzo: sabahionline.com
No comments:
Post a Comment