Askari
akijihami wakati wa vurugu kubwa zilizozuka leo majira ya jioni Jiji la
Mombasa wakati Waumini wa dini ya Kiislamu wa Msikiti 'Masjid Mussa'
ambapo waumini hao wamedaiwa kuwa walikuwa wameandaa mkutano wa hadhara
waliouita Kongamano ambalo Serikali ilikataa kuwepo kwa muhadhara huo
na wao kupinga maamuzi hayo.
Imeelezwa
kuwa Baada ya kukatazwa kufanya muhadhara huo, waliamua kuweka Bendera
ya Kiislamu katika Msikiti huo huku wakitoa 'Fatwa' kuwa kuanzia leo
hawaitambui Bendera ya Kenya, jambo ambalo lilipelekea kutokea kwa
vurugu hizo baina ya Askari na waumini hao. Aidha imeripotiwa kuwa watu
kadhaa wamefariki dunia katika vurugu hizo na wengine kujeruhiwa.
Polisi wakiwadhibiti waumini wa dini ya kiislamu jijini Mombasa, nchini Kenya
Mmoja kati ya waumini hao akiwa hoi baada ya kujeruhiwa katika vurugu hizo.
Mmoja wa majeruhi
No comments:
Post a Comment