Wajumbe wa waasi wa Sudan Kusini katika mazungumzo ya kusaka amani, januari 13 mwaka 2014 mjini Addis-Ababa.. |
Serikali
ya Ethiopia ambayo inasimamia mazungumzo ya waasi wa Sudani Kusini na
serikali ya rais Salva kiir imetowa wito wa kuondolewa kwa majeshi ya
Kigeni nchini Sudani Kusini hususan majeshi ya Uganda kwa hofu ya
kuufanya mzozo huo kuwa wa kikanda.
Waasi wa
Sudani Kusini wametishia kujiondowa kwenye mazungumzo hayo iwapo
wanajeshi wa Uganda wataendelea kutekeleza mashambulizi dhidi ya vikosi
vyao.
Majeshi ya Uganda yaliingia nchini Sudani Kusini kufuatia ombi la rais Salva Kiir kukabiliana na waasi.
Taban
Deng mjumbe wa waasi kwenye mazungumzo hayo amesema katika taarifa
iliotolewa jana kwamba watajiondowa kwenye mazungumzo hayo iwapo majeshi
ya Uganda yatasalia nchini Sudani Kusini huku akitowa wito wa kuachiwa
huru wafungwa wanne ambao bado wanazuiliwa katika jela moja jijini Juba.
Taifa
changa la Sudan Kusini limekua katika mapigano kati ya jeshi la serikali
na waasi wanaomuunga mkono aliekua makamu wa rais Salva Kiir, Riek
Machar, tangu desemba 15 mwaka jana.
Mapigano hayo yalisababisha mamia ya raia kupoteza maisha na mamia kwa maelfu wamelazimika kuyahama makaazi yao.
Mazungumzo
yanayoendelea mjini Addis-Ababa, nchini Kenya yameanzishwa kwa jitihada
za Jumuiya ya Kikanda ya maendeleo ya Afrika ya Mashariki IGAD.
Awali
serikali ya Uganda ilikataa katu katu kwamba haikuwatuma wanajeshi wake
nchini Sudan Kusini, lakini siku chache baadae, serikali hio ilikiri
kuwatuma wanajeshi wake kwenye aridhi ya Sudan Kusini ili kusidia jeshi
la seikali linalomuunga mkono rais Salva Kiir.
Via kiswahili.rfi.fr
No comments:
Post a Comment