Pages

Friday, February 7, 2014

Waisilamu hatarini mji wa Bangui, CAR


Licha ya Rais wa mpito kuapishwa hali CAR bado ni tete
Maelfu ya waislamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekuwa wakiondoka katika mji mkuu wa taifa hilo Bangui mapema leo.
Wakiwa wameabiri malori na kusindikizwa na wanajeshi wa taifa la Chad,ni msafara wa hivi karibuni wa waislamu kutoroka vita wakiwa na matumaini ya kupata hifadhi katika taifa jirani la Chad.
Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka Medical San Frontiers limeshtumu kile linachokitaja kuwa ghasia za kupita kiasi dhidi ya waislamu walio wachache.
Walioshuhudia wameelezea kuwa ni msafara mkubwa kuwahi kuonekana nchini humo katika siku za hivi karibuni.
Maelfu ya waislamu tayari wameondoka katika mji huo na kuelekea nchini Chad na Cameroon.
Makaazi yote yaliokuwa yakimilikiwa na waislamu katika mji mkuu wa Bangui pamoja na miji mingine yamebakia kuwa mahame.
Katika maeneo mengine makundi ya waislamu yametengwa huku yakitishiwa na wanamgambo wa kikristo.Barabara inayoeelekea mpakani haina usalama kwa kuwa misafara pia huvamiwa.
Shirika la madaktari wasio na mipaka MSF linasema kuwa familia za kiislamu zinalazimishwa kwenda mafichoni ili kuepuka maafa.
Linasema kuwa idadi kuu ya wakristo pia imeathiriwa na vita hivyo ambavyo vimefikia viwango vibaya.Wanadiplomasia wanahofia kwamba huenda jamii ya waislamu nchini humo ikatoweka.
Makaazi na misikiti yameharibiwa na kuchomwa.

No comments:

Post a Comment