Kamati
ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungia
mechi tatu wachezaji watano kati ya tisa wa timu ya Kanembwa JKT
waliolalamikiwa na Sekretarieti kwa kumpiga mwamuzi kwenye mechi ya Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) iliyochezwa Novemba 2 mwaka jana.
Wachezaji
hao ni Bariki Abdul, Mrisho Musa, Nkuba Clement, Nteze Raymond na Philo
Ndonde. Wachezaji ambao hawakutiwa hatiani kutokana na ushahidi dhidi
yao kutojitosheleza ni Abdallah Mgonja, Mbeke Mbeke, Ntilakigwa Hussein
na Uhuru Mwambungu.
Mechi
hiyo dhidi ya Stand United iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga ilivunjwa na refa Peter Mujaya dakika ya 87 kutokana na
kupigwa na wachezaji hao baada ya kuamuru ipigwe penalti dhidi ya timu
yao.
Adhabu
hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya 49 (1)(b) ya Kanuni za Nidhamu
za TFF baada ya kupitia vielelezo vilivyowasilishwa na Sekretarieti ya
TFF ambavyo ni ripoti ya refa, ripoti ya kamishna wa mechi hiyo na video
iliyoonesha tukio hilo.
Pia
kabla ya kutoa adhabu baada ya kusikiliza utetezi kutoka kwa
walalamikiwa ambao ni wachezaji hao na timu yenyewe ya Kanembwa JKT.
Nayo Kanembwa JKT imetiwa hatiani na kupigwa faini ya sh. milioni ambayo
inatakiwa kuilipa kabla ya kucheza mechi inayofuata.
Kamati
hiyo iliyokutana jana (Februari 9 mwaka huu) chini ya Mwenyekiti wake
Tarimba Abbas, kwanza imelaani kitendo cha wachezaji wa timu hiyo
kumzonga refa, kwani vitendo vya aina hiyo ndiyo vichocheo vya vurugu
viwanjani.
Lakini
pia imempongeza nahodha wa Kanembwa JKT, Mbeke Mbeke kwa kuwa mstari wa
mbele kuwazuia wachezaji wenzake waliokuwa wakimpiga refa wa mchezo huo.
Vilevile
Kamati hiyo imesema aliyesababisha matatizo hayo ni refa Mujaya, na
ingawa ilikuwa na uwezo wa kumchukulia hatua lakini haikufanya hivyo kwa
vile hakukuwa na mlalamikaji na tayari Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
ilishamwadhibu.
No comments:
Post a Comment