Vijana walioghadhabishwa na
tukio la polisi kuvamia msikiti mmoja unaotumiwa na wahubiri
wanaosemekana kuhubiri itikadi kali za kiisilamu mjini Mombasa,Pwani ya
Kenya, wamekabiliana na polisi kwa siku ya pili leo.
Duru zinasema kuwa Maafisa wa usalama wanakutana
kujadili matukio ya Jumapili mjini Mombasa ambapo polisi waliwakamata
vijana katika msikiti wa Musa .Msako wa polisi ulisababisha vifo vya watu watatu akiwemo polisi mmoja huku wengine wengi wakijeruhiwa.
Polisi walichukua muda wa masaa tatu kuendesha msako, katika msikiti wa Musa mtaani Majengo baada ya kupata habari kuwa mkutano wa vijana kuhusu jihad ulikuwa unaendelea ndani ya msikiti huo.
Zogo lilianza baada ya vijana waliokuwa ndani ya msikiti huo unaohushwa na marehemu Aboud Rogo kuzuia polisi kuingia ndani. Watu watatu waliuawa na wengine kujeruhiwa wakati polisi wakifanikiwa kuwakamata vijana karibu miamoja.
Miongoni mwa waliokamatwa alikuwa mwanawe marehemu Rogo aliyesema kuwa wakati walipokamatwa kulikuwa na bunduki 18 ndani ya msikiti huo na kuwa alihadaiwa kuhudhuria mkutano huo.
Taarifa zinasema kuwa mkutano huo wa vijana uliandaliwa kupitia mitandao ya kijamii huku vijikaratasi vikisambazwa mjini humo kuwaalika watu.
No comments:
Post a Comment