Pages

Friday, March 28, 2014

ASKOFU WA DAYOSISI YA CENTRAL TANGANYIKA, GODFREY MHOGOLO AFARIKI


ASKOFU wa Dayosisi ya Central Tanganyika, Godfrey Mhogolo amefariki
dunia leo Nchini Afrika Kusini alikokuwa amekwenda kwa matitabu..
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kanisa la Angilikana Dodoma jana,
ilisema kuwa Askofu Mhogolo kabla ya kufikwa na mauti alikuwa
akitibiwa katika hospitali ya Milpark huko Johanesburg, Afrika Kusini.
Askofu Mhogolo alikuwa askofu wa tano wa dayosisi ya Central
Tanganyika na atazikwa katika viwanja vya kanisa Kuu la Roho Mtakatifu
Mjini Dodoma.
Hata hivyo Mchungaji Michael Nchimbi alisema mipango ya mazishi
inaendelea na taarifa zitatolewa baadaye.

No comments:

Post a Comment