Pages

Tuesday, March 25, 2014

BASATA YAZITOA NYIMBO ZA JUX,SNURA NA MADEE KUWANIA TUZO ZA KTMA 2014

Kili Photo

Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey L. Mngereza (katikati) akiongea na waandishi wa habari
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) leo limetangaza rasmi matokeo ya mchakato wa kuwapata wateule rasmi wa vipengele 34 vya tuzo za muziki Tanzania. Akiongea na waandishi wa habari, Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey L. Mngereza amesema zaidi ya mapendekezo 30,000 yalitumwa kwa njia ya sms na mtandaoni. Hata hivyo alidai kuwa nyimbo ‘Uzuri Wako’ ya Jux, Nimevurugwa ya Snura na Tema Mate Tuwachape ya Madee zimeondolewa kwenye mchakato huo kwa madai kuwa zimevunja maadili na hazifai kwa jamii ya Kitanzania

No comments:

Post a Comment