Wakazi wa Kiwangwa, wa Kiwangwa, wakivushwa na vijana waliojitolea kujipatia ajila katika Daraja la Ruvu kwa kuwavusha wananchi kwa kuwabea ama kuwaongoza njia ili kuvuka eneo hilo la daraja lililojaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini. Kamera ya Sufianimafoto iliwashuhudia viajana hao wakiwavuja raia katika eneo hilo kwa ujila wa Sh. 2000 kwa kila aliyebebwa mgongoni asiyetaka kuvua viatu ama kugusa maji hayo, na Sh. 500 kwa kushikwa mkono kuongozwa njia kutoka mwanzo wa maji hayo hadi kuyavuka, na kuyaongoza magari kuvuka eneo hilo ni Sh. 3000 hadi 5000.
Kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jana, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, alifika eneo hilo na kujionea wananchi wakitaabika kuvuka ene hilo na huku magari ya abiria yaliyokuwa yakitokea Bagamoyo kwenda Kiwangwa, yakibeba abiria na kuishia eneo hilo na kubeba wengine walioshushwa upande wa pili na kugeuza kwa kila abiria kulipa Sh. 1000. Na kisha abiria hao wakipata usafiri mwingine wa kubebwa na Vijana waliopo eneo hilo kwa Sh. 2000 kwa aliyependa ama 500 kwa kuongozwa njia.
Vijana hao wakiliongoza moja ya gari lililokuwa likivuka eneo hilo ambapo dereva anafuata njia wanayopita vijana hao wa kulia na kushoto hadi kuvuka ili kuoepuka kupita eneo hatarishi na kutumbukia ama kusukumwa na maji hayo yaliyokuwa yakionekana kuwa na nguvu kubwa.
Mkuu wa Wilaya ya bagamoyo, Ahmed Kipozi, akizungumza na watendaji wake aliowaagiza kusimamia zoezi la kuwazuia wananchi kuvuka eneo hilo, ambapo watendaji hao walimueleza Mkuu huyo wa Wilaya kuwa wananchi wamekuwa wakaidi na kuamua kukataa kutii amri na kuvuka, jambo lililomfanya Mkuu wa wilaya kuamua kuagiza askari Polisi wenye silaha ili kulinda eneo hilo kuwazuia waanchi kuvuka ili kuepuka maafa.
''WA HUKU WA HUKU NA WA HUKO WA HUKO''
Baada ya hapo Mkuu huyo wa Wilaya aliwatoa tamko na kuwataka wakazi wa Kiwangwa kutokwenda Bagamoyo na waBagamoyo kutokwenda Kiwangwa, kwa kipindi chote cha mvua ili kuepuka maafa yanayoweza kutokea kwa kutumbukia na kusombwa na maji, ama daraja hilo la Jeshi kukatika kutokana na maji kuanza kupita juu ya daraja hilo jana.
Mkuu wa Wilaya, akizungumza na madereva wa magari waliokuwa wakisubiri kuvuka eneo hilo pamoja na vijana waliokuwa wakitoa huduma ya kuwavusha watu.
Baadhi ya magari yaliyokaidi amri yakivuka eneo hilo.
Vijana hao waliwavusha hadi wagonjwa katika eneo hilo kama anavyoonekana pichani akiwa amembeba mtu mzima anayeonekana kuwa ni mgonjwa.
Baadhi ya vijana walijiona kama wapo Beach, walikuwa wakipiga mbizi na kuogelea eneo hilo kwa furaha.
Magari yakiwa katika foleni kusubiri kuvuka eneo hilo.
Baadhi ya abiria walioshushwa upande wa pili wakiwania usafiri wa kuelekea Bagamoyo baada ya kufaulishwa na gari jingine la uapnde wa pili.
Hawa nao ni wa upande wa pili
Gari la Abbas Tarimba likivuka eneo hilo.
Vijana wakijipigia debe kwa dereva ili akibali kuvushwa, bila kujua kuwa ndani yake alikuwapo Mkuu wa Wilaya hiyo.
Katapila lililoletwa ili kuziba eneo hilo kuzuia magari kuvuka....
Haya ni baadhi ya madaraja ya barabara mpya inayojengwa yakiwa yamejaa maji.
Dereva wa pikipiki akipakia gunia la mkaa vizuri ili awapakie na abiria wake wawili baada ya kuvuka darajani hapo.
Haya ni baadhi ya maeneo hayo yaliyojaa maji, ambapo mmoja wa vijana hao anaonekana akipiga mbizi kwa furaha.
'Bonge' la Mgahawa likiwa limejaa maji
Pembeni (kulia) ni mtumbwi unaotumiwa na wakazi wa eneo hili kuvuka kuelekea upande wa pili.Chanzo Sufiani Mafoto.com
No comments:
Post a Comment