Theluthi
ya idadi ya watu wote duniani haina access na Internet. Facebook tayari
ina zaidi ya watumiaji bilioni 1, lakini kabla haijampata kila mtu
duniani ni lazima kila mmoja awe na access na internet.
Kampuni
hiyo ya mtandao wa kijamii imetangaza hatua mpya katika hamu yake ya
kupeleka internet isiyo na gharama kwa kila mtu duniani.
Maabara
mpya ya Facebook kuhusu upatikanaji wa internet itafanya utafiti na
kujaribu teknolojia ya ndege zisizotumia rubani (drones) pamoja na
satellite kusambaza huduma ya internet katika maeneo ambayo hayana kwa
sasa.
“Tumekuwa tukifanyia kazi njia ya kuwapa watu internet kutoka angani,” alisema CEO wa mtandao huo, Mark Zuckerberg.
Teknolojia
hiyo itahusisha ndege hizo zitakazokaa angani kwa miezi kadhaa na
kuwapa watu internet katika maeneo ya mbali. Kufanikisha hilo, Facebook
imechukua wataalam kutoka NASA na timu iliyotengeneza ndege ya Zephyr
inayotumia jua.
Soma zaidi hapa.
No comments:
Post a Comment