Pichani
juu na chini ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza
na wakazi wa Halamshauri ya mji mdogo wa Namanyere Wialayani Nkasi
jioni ya jana,kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika nje ya uwanja wa
Ofisi za chama hicho.Kinana alieleza kuwa kufuatia na taarifa
mbalimbali alizokabidhiwa na Viongozi wa chama wilayani humo,alieleza
kuwa wilaya ya Nkasi ina kero kadhaaa ikiwemo suala la Maji,Umeme,Uhaba
wa walimu,Barabara pamoja na tatizo la soko la kuuza mazao ya
wakulima,Kinana ameahidi yote hayao kuyafannyia kazi kwa kuhakikisha
utekelezaji unafanyika kwa namna moja ama nyingine.
Baadhi
ya Wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana wakisikiliza kwa makini huku na wao wakiandika mambo
kadhaa yaliyokuwa yakizungumza na Kinana kwa ajli ya kuweka kumbukumbu.
Mwenyekiti
wa CCM,Mkoa wa Rukwa,Ndugu Hypolitus Matete akimtambulisha Mjumbe wa
Halmashauri kuu ya Taifa,kutoka Zanzibar,Balozi Ali Abeid karume kwa
wananchi halmashauri ya mji mdogo Namanyere,wilayani Nkasi mkoani
Rukwa,kwenye mkutano wa hadhara.
Moja
ya Kikundi cha ngoma za asili cha halmashauri ya mji mdogo,Namanyere
Wilayani Nkasi wakitumbuiza kwenye mkutano wa hadhara uliondaliwa na
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana aliyewasili leo wilayani humo mkoani
Rukwa kwa ziara ya kichama mkoani Rukwa.
Baadhi
akina mama wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa
hadhara uliofanyika nje ya uwanja wa ofisi za sisi,wilayani Nkasi mapema jana jioni
Wanachama
mbalimbali wa CCM na wananchi waliofika kwenye mkutano huo wa
hadhara,wakishangilia jambo.Ambapo katika mkutano huo Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana aliwahutubia wananchi wa halmashauri ya mji mdogo wa
Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa jioni ya jana.
Baadhi ya wananchi wakishangilia jambo
chanzo michuzijr
No comments:
Post a Comment