Ndege na meli za Australia
zimeanza siku ya tatu kufanya msako katika bahari hindi ambako waziri
mkuu wa nchi hiyo alisema mabaki yanayoaminika kuwa ya ndege ya Malaysia
iliyopotea wiki mbili zilizopita yalionekana.
Mawimbi ya bahari yametulia na hali ya anga inasemekana kuwa nzuri zaidi kuliko siku mbili zilizopita.Ndege hiyo, ilitoweka wiki mbili zilizopita, ikiwa na abiria miambili na arobaini. Ndege zaidi kutoka China na Japan zinatarajiwa kujiunga na msako huo katika siku chache zijazo.
Msako huo umeingia wiki yake ya tatu , lakini hakuna kilichopatikana kuongeza matumaini kuwa ndege iko salama.
Ndege hiyo MH370, ilipoteza mawasiliano ilipokuwa njiani kutoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing tarehe 8 mwezi Machi.
Maafisa nchini Malaysia wanashuku kwamba mawasiliano ya ndege hiyo yalikatizwa kwa maksudi.
No comments:
Post a Comment