Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, March 9, 2014

MAMA ASHA BILAL ALIPOTEMBELEA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YALIYOANDALIWA NA 8020 Fashions


 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Asha Bilal (kulia) akibonyeza kitufe kufungua maonesho ya kazi za wanawake wakati wa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani zilizofanyika leo ukumbi wa Diamond Jubilee hall jijini Dar es salaam. Kushoto ni mwandaaji wa maonesho haya Bi. Shamim Mwasha ambaye ni mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya 8020 Fashions (http://www.8020fashionsblog.com/)
 Mama Asha Bilal akiingia kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee  wakati wa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani zilizofanyika leo. Kushoto ni mwandaaji wa hafla hiyo Bi. ShamimMwasha wa 8020 Fashions na kulia ni mama wa Mitindo Asia Idarous-Khamsin
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Asha Bilal  akiwa meza kuu  pamoja na waandaaji na wake wa Viongozi mbalimbali kwenye Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo 
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Asha Bilal, akihutubia kwenya hafla hiyo
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Asha Bilal, akikagua kazi mbalimbali za wanawake kwenye hafla hiyo
  Mama Asha Bilal akiangalia kazi mbalimbali za wanawake kwenye hafla hiyo
 Mama Asha Bilal akiwapongeza wanawake walioonesha kazi zao  kwenye hafla hiyo
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Asha Bilal, akimkabidhi cheti mmnoja ya wadhamini wa shughuli ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyoandaliwa na kampuni ya 80-20 Fashen ya Sinza jijini Dar es salaam bibi Mwanjaa Serabe Meneja wa mpango wa uchangiaji wa hiyari wa PSPF  yaliyofanyika leo  katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
 Malkia wa Taarab Khadija Omar Kopa akitumbiza kwenye Maadhimisho ya siku wa Wanawake Duniani katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
 Mama Asha Bilal akiwa katika picha ya pamoja na wake wa Viongozi mbalimbali kwenye Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo. Picha na OMR


 

No comments:

Post a Comment