Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, March 8, 2014

NDEGE YA MALAYSIA AIRLINE INADAIWA KUDONDOKA KATI YA VIETNAM NA TAILAND ILIKUWA NA WATU 239

Ndugu wa abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo wakisubiri taarifa kuhusiana na ndege hiyo
Ndege ya Malaysia Airlines iliyokuwa na abiria 227 na wafanyakazi 12 inahofiwa kuanguka huko katika bahari kusini mwa China, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la Vietnam.
Ndege hiyo aina ya Boeing 777-200ER iliyokuwa inatoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing, ilikuwa imepotea kwa masaa kadhaa. Kama ripoti hiyo ikithibitisha, itakuwa ni ajali mbaya ya ndege ya aina hiyo (Boeing 777) tangu iingie sokoni miaka 19 iliyopita.

Ndugu wakifanya mawasiliano kutaka kujua ukweli
Malaysia Airlines bado haijathibitisha iwapo ndege hiyo imeanguka.

No comments:

Post a Comment