Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, March 26, 2014

Redd's Original yawapiga msasa waandaaji wa shindano la Miss Tanzania 2014

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency ambao ndio waandaaji wa shindano la Redds Miss Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza na mawakala wa shindano hilo Dar es Salaam jana katika semina ya seku mbili. Katikati ni Redd's Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa na Mshindi wa pili, Latifa Mohamed. Shindano la Miss Tanzania linadhaminiwa na Kinywaji cha Redd's Original.
 
 Baadhi ya mawakala wa shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakiwa  katika semina ya siku mbili juu ya namna ya ufanyanyaji wa mashindano hayo mwaka huu jijini Dar es Salaam jana. Shindano la Miss Tanzania linadhaminiwa na Kinywaji cha Redd's Original.
========  ======  ====
MAWAKALA wa mashindano ya urembo nchini wametakiwa kutafuta washiriki wenye vigezo kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo mwaka huu na hatimaye kupata mshindi wa kitaifa “Redd’s Miss Tanzania 2014” atakayeipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye fainali za dunia.
Akizungumza katika semina ya mawakala hao iliyofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Regency iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Lino Agency International, Hashim Lundenga, aliwataka kusaka washiriki bila ya kuwanyanyapaa wasichana kutokana na maumbile yao.
Lundenga alisema kuwa mawakala hawapaswi kutoa maamuzi ya washiriki wakati wa mchakato wa kutafuta warembo na jukumu la kufanya hivyo litabaki kwa majaji.
Mkurugenzi huyo alisema pia mawakala wanaume wanatakiwa kuwa makini katika mchakato huo wa awali na kuhakikisha wanaendeleza maadili ya Kitanzania na kufanikisha sanaa hiyo inazidi kufanikiwa.
“Si vizuri kuwakataa wasichana wanaotaka kushiriki kwa sababu eti wafupi au sabau nyingine…kufanya hivyo si sahihi, pia huu ni wakati mwingine kwa mawakala wanaume kuhakikisha mnavivuka  viunzi kwa wasichana wanaojiandaa kuwaweka mtegoni,” alisema Lundenga.
Aliwataka mawakala hao pia kuhakikisha wanafanya mazungumzo na makampuni na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kusaka udhamini wa kufanikisha mashindano yao ambayo yanaania ngazi ya vitongoji, wilaya, mikoa na kanda.
“Kuhusiana na zawadi pia mnatakiwa kuwa na makubaliano na washiriki kulingana na uwezo wako wakala…hata kama uko tayari kutoa jiko waeleze hivyo,” Lundenga aliongeza.
Aliwaeleza pia mawakala hao kwamba mdhamini mkuu wa mashindano hayo ni Redd’s Original ambayo imeahidi kutumia zaidi ya Sh. Milioni 500.

Happiness Watimanywa ndiye mrembo anayetetea taji la taifa na mshindi wa pili, Latifa Mohammed pia walikuwepo jana katika semina hiyo inayotarajiwa kumalizika leo

No comments:

Post a Comment