Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, March 11, 2014

UELEWA MDOGO WA WANANCHI JUU YA UENDELEZAJI WA MIRADI INAYOANZISHWA UMEPELEKEA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA MAJI NA MAENDELEO MAMADO KUCHELEWA KUTEKELEZA MIRADI YAKE.





Akizungumza na Dodoma FM Meneja Mipango wa Shirika la MAMADO Bwana  Agustino Rukeha amesema pamoja na shirika hilo  kutoa Elimu ya uendelezaji wa miundombinu  bado jamii haijajenga dhana ya kujitolea kuchangia kuendeleza miradi inayoanzishwa na mashirika mbalimbali.
Aidha Bwana Rukeha amesema pamoja na shirika hilo kufanya kazi kwa kufuata sera ya nchi ya wananchi kuchangia lakini bado jamii imekuwa haina uelewa wa kutosha  katika suala la kuchangia.
Nae Kaimu Meneja Mipango wa shirika hilo Bwana Ernest Mella amesema miradi mingi imekuwa ikichelewa kutokana na ushiriki mdogo wa jamii  kwani wananchi wamekuwa hawana uelewa wa kutosha juu ya uendelezaji wa miradi

No comments:

Post a Comment