Pages

Friday, March 28, 2014

WAZIRI MKUU MHE. PINDA NA VIONGOZI WA SERIKALI WAHUDHURIA IBADA YA KUMWOMBEA HAYATI TUPA


Mchungaji akiombea Safari ya Mwili wa Marehemu Jonh Gabriel Tuppa (aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara) Kutoka Mkoa wa Mara Kueleka Morogoro Kwaajili ya Mazishi.

 Jeneza lilobeba Mwili wa Marehem John Gabriel Tuppa likiwa Viwanya vya Nyerere Square Mjini Dodoma mara baada ya Kuwasili Ukitokea Mkoa wa Mara kuelekea Mororgoro Kwa Mazishi.
Viongozi wa Serikali Waliofika Kuuga Mwili wa Marehemu Tuppa wakiongozwa na Mh:Waziri Mkuu wakiwa kwenye Maombi ya Kumuombea Marehemu apumzike kwa Amani.

Kikosi cha Askari kilichobeba Mwili wa Marehemu Tuppa na Kuuleta Viwanya Vya Nyerere Square kwaajili ya Kuuagwa na Viongozi wa Serikali waliopo Dodoma,Pia Marehemu alipata Kuwa Mkuu wa Wilaya Dodoma Mjini enzi za Uhai Wake.Familia ya Marehemu John Tuppa wakiongozwa na Mke wa Marehemu Tuppa wa Pili kutoka Kulia wakiwa wamewasili Viwanja Vya Nyerere Square Mjini Dodoma hii leo.'

 Mke wa Marehemu Mama Tuppa akisalimiana na Viongozi wa Juu wa Serikali Mh;Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais Mh:Balozi Seif Idd Viwanja Vya Nyerere Square hii leo.

Kwaya ya Parokia ya Dodoma Mjini Wakiimba wakati wa Misa ya Kuuga Mwili wa Marehemu Tuppa Mjini Dodoma hii leo.


Sehemu ya Waombolezaji waliofika Viwanya Vya Nyerere Square kwaajili ya Kushiriki tukio la Kuuga Mwili wa Marehemu Tuppa ambaye katika Enzi za Uhai wake aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya Dodoma Mjini.Mke wa Marehemu John Gabriel Tuppa akifarijiwa na Wafiwa Wengine

 Mh.Lukuvi(mbunge wa Isimani-Iringa) akibadilishana Mawazo na Waziri  Mkuu Mstaafu Mh:Edward Lowassa wakati wa tukio la Kuuaga Mwili wa Marehemu John Gabriel Tuppa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara hii leo Dodoma.

Misaa inaendelea ya Kuuga Mwili wa Marehemu Tuppa.

 Baadhi ya Viongozi wa Serikali waliohudhuria tukio la Kuuaga Mwili wa Marehemu Tuppa Mjini Dodoma hii leo.

Mwenyekiti wa Wazee Mkoa wa Dodoma akitoa Salamu za rambirambi kwa Wafiwa na Waombolezaji wakati wa Kuuga Mwili wa Marehemu Tuppa hii leo Mjini Dodoma.

 Naibu katibu Mkuu CCM_Bara Mh:Mwigulu Lameck Nchemba akitoa Salamu za Rambirambi za Chama Cha Mapinduzi.

Muwakilishi Kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma akitoa Salamu za Rambirambi kwa Wafiwa.Marehemu Tuppa enzi za Uhai wake alisaidia sana wakati wa Ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma wakati huo akiwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini.

 Bi.Neema Sitta Muwakilishi wa Food World Program akitoa Salamu za Rambirambi,aliwahi kufanya kazi na Marehemu Tuppa Mkoani Mara.

Katibu wa BAKWATA Mkoa Wa Dodoma akitoa Salamu za Rambirambi kutoka Dini ya Waislamu kwa Wafiwa.

 Baba Askofu Dayosisi ya Dodoma akitoa Salamu za Rambirambi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rehema Nchimbi akitoa Salamu za rambirambi kwa niaba ya Serikali Mkoa wa Dodoma.

 Mh:Lukuvi(Mb) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya CDA akitoa Salamu za Rambirambi Kwa Marehemu John Tuppa.'

Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wanawake (UWT) Mh:Amina Makilagi akiwa katika Uso wa Huzuni kuomboleza Kifo cha Marehemu.John Tuppa.Taji likiletwa Mbele ya Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu John Gabriel Tuppa.Mwanga wa Bwana Ukuangazie Milele.

 Makamu wa Pili wa Rais Mh:Balozi Seif Idd akitoa heshima ya Mwisho Kwa Marehemu John Gabriel Tuppa hii leo Mjini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh:Mizengo Pinda kitoa Heshima ya Mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Gabriel Tuppa hii leo wakati wa Kuuga Mwili huo Mjini Dodoma kabla ya Kuondoka kuelekea Morogoro kwa Mazishi.

 Mama Anne Semamba Makinda Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania akitoa Heshima ya Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Tuppa.

Mh:Masatu Wasira akitoa Heshima ya Mwisho kwa Marehemu Tuppa.

 Waziri Mkuu Mstaafu Mh:Edward Lowassa akitoa Heshima ya Mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Tuppa hii leo Dodoma Mjini.

Mh:Lukuvi akitoa Heshima ya Mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Tuppa.

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rehema Nchimbi akitoa Heshima ya Mwisho kwa Marehemu Tuppa.

Mh:Zakhia Meghji akitoa Heshima ya Mwisho kwa Marehemu Tuppa.

 Mh:Job Ndugai Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri la Tanzania akitoa Heshima ya Mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Tuppa.

Naibu katibu Mkuu na Naibu waziri wa Fedha na Uchumi Mh:Mwigulu Nchemba akitoa Heshima ya Mwisho kwa Marehemu John Tuppa.

 Mwili wa Marehemu John Gabriel Tuppa hii leo Umefika Dodoma kwaajili ya Kuagwa na Wananchi wa Dodoma na Viongozi wa Serikali walipo Dodoma ukitokea Mkoa wa Mara.Marehemu Tuppa alifariki Ghafla Tar.26/03/2014 Wilayani Tarime akiwa kazini.Mwili wake Umesafirishwa Kuelekea Mkoani Morogoro kwaajili ya Mazishi.

Picha/Maelezo na Vijimambo blog

No comments:

Post a Comment