Watu 29 wamejeruhiwa katika ajali mbili
tofauti zilizotokea katika barabara kuu ya Morogoro-Dar es Salaam
kwenye maeneo ya Mikese na Mkambalani, mkoani hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,
Faustine Shilogile alithibitisha kutokea kwa ajali hizo na kusema
zilihusisha mabasi ya abiria; moja likiwa basi la Nganga lililokuwa
likitoka Dar es Salaam kwenda Mbeya na la Sumry lililokuwa likitoka
Tunduma.
Ajali ya kwanza ambayo majeruhi ni 15 saa 2:30 usiku, ilitokea juzi eneo la Mkambalani, Morogoro Vijijini.
Ilihusisha basi la kampuni ya Sumry yenye
namba za usajili T 888 BWK . Ilikuwa ikiendeshwa na Muhina Mohamedi
(39) mkazi wa Mbeya ikitoka Tunduma kwenda Dar es Salaam.
Basi hilo liligongana uso kwa uso na basi
dogo la abiria aina ya Coaster yenye namba za usajili T273 CCV ambayo
dereva wake hakufahamika. Ilikuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Mbeya.
Chanzo cha ajali kilitokana na basi la Sumry kutaka kupita gari la mbele yake.
Kwa upande wa ajali ya basi la Nganga
lenye namba za usajili T252 AZU, ilikuwa ikiendeshwa na Alex Eliya (49)
mkazi wa Misufini mkoani kabla ya kupasuka tairi la mbele kulia na
kupoteza mwelekeo kisha kupinduka.
Idadi ya majeruhi katika ajali hiyo ni 14
ambao walipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro. Ajali hiyo
ilitokea jana saa 3:30 asubuhi katika eneo la Miembeni Mikese, Wilaya
ya Morogoro.
Baadhi ya majeruhi wa ajali hizo, akiwemo
Esau John na Jane Lawa waliokuwa kwenye basi hilo la Nganga, walisema
kilichosaidia kutokuwepo vifo ni kwa kuwa basi halikuwa kwenye mwendo wa
kasi.
Mganga wa zamu katika hospitali hiyo ya
mkoa, Dk Alex Makala, alisema jana walibaki majeruhi 12 baada ya wengine
kutibiwa na kuruhusiwa kutokana na kuwa na majeraha madogo.
BOFYA HAPA LIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGII ZA KILA KONA
BOFYA HAPA LIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGII ZA KILA KONA
No comments:
Post a Comment