WATU 14 WAFARIKI KATIKA AJALI
MKOANI SINGIDA USIKU WA KUAMKIA LEO WATU 13 akiwemo askari wa kikosi cha usalama
barabarani wamepoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya
Sumry lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar katika kijiji cha Ikungi
mkoani Singida usiku huu.
Ajali hiyo ilitokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori
lililomgonga mwendesha baiskeli aliyepoteza maisha papo hapo na wakati
wananchi wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea
kupima ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry na kuwagonga watu
hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 14 kupoteza maisha
eneo hilo.
Basi hilo lililokuwa likitokea Kigoma kwenda Dar halikuweza kusimama
eneo hilo mpaka dereva wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi
Ikungi, Singida. Miili 14 ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo
imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja na majeruhi
wawili waliopelekwa hospitalini hapo.
No comments:
Post a Comment