Watu
19 wa kijiji cha Utaho wilayani Ikungi wamepoteza maisha wakiwemo
askari wanne wa jeshi la polisi, baada ya kugongwa na basi la Summry
wakati wakiwa wana toa msaada wa kumpakia marehemu kwenye gari la polisi
aliye gongwa na gari kubwa ambalo halikufahamika mara moja .
Basi hilo la kampuni ya Sumry hufanya safari zake
kati ya Kigoma na Dar-es-salaam. Dereva wa basi hilo alikimbia mara tu
na baada ya ajali hiyo na kulitekeleza basi hilo.
Mwandishi wa habari wa ITV alifika na kuwakuta
wasafiri walionusurika wakiwa katika kituo cha polisi cha Ikungi bila
ya kujua hatima yao ya safari baada ya basi lao kuwakanyaga na kuuwa
watu 19
PICHA ZOTE NA :Elisante Mkumbo-Singida
Gari
la polisi likiwa limepakia maiti zaidi ya kumi zikipelekwa hospitali ya
mkoa wa singida kwa ajili ya kuhifadhiwa na kutambuliwa
No comments:
Post a Comment