Mwanamume mmoja nchini Kenya aliwaacha wakazi wa
kijiji cha Tivani mkoa wa Bonde la uffa vinywa wazi baada ya kujichimbia
kaburi na hata kujaribu kujizika mwenyewe kutokana na alichosema ni
matatizo ya ndoa.
Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha KTN nchini
Kenya, tukio hilo lililotokea Jumanne asubuhi na kuwashangaza wakazi wa
eneo la Trans Nzoia mkoa wa Rift ValleyMwanamume huyo, alidai kuwa ana matatizo ya ndoa ambayo yeye mwenyewe ameshidwa kuyatatua na kwa hivyo kwake kilichosalia ni kwenda mbinguni.
Alisema mkewe alikuwa amemwambia jambo ambalo lilimkera roho na ndhio maana akaamua kujitoa uhai.
Mwanamume huyo kwa jina Kipsang , alichimba kaburi hilo usiku na hata kujaribu kujizika akiwa hai wakati mkewe na watoto wake walipokuwa wanalala.
Wanakijiji katika kijiji cha Tivani walikuwa na wasiwasi kuwa mwanamume huyo alikuwa amerukwa na akili ingawa walikiri kwamba yeye na mkewe wamekuwa wakikumwba na matatizo ya ndoa.
Mkewe alisema kuwa amechoshwa na mwanamume huyo ambaye ametelekeza familia na majukumu yake.
Baba huyo wa watoto wawili ambaye ni kondakta wa matatu, hatimaye aliondoka katika kaburi hilo baada ya wanakijiji kumsihi huku wazee wakiwataka watu kupanda migomba ya Ndizi neneo alilokuwa amechimba kaburi hilo ili kuzuia mikosi.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment