Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema nchi ya Jamuhuri ya Kati haipaswi kuruhusiwa kugeuka kuwa Rwanda nyingine.
Akiandika
maoni yake kwenye mtandao wa BBC, Bwana Ban amesema kwamba zaidi ya
nusu ya raia wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati wanahitaji msaada wa
kibinadamu.
Akihusisha
mambo yalivyo Jamuhuri ya Afrika ya Kati na kumbukumbu ya miaka 20 ya
mauaji ya halaiki nchini Rwanda, amesema jamii ya kimataifa inapaswa
kuchukua hatua sasa badala ya baadae kuja kuomba msamaha itakapotimia
miaka ishirini ijayo.
Siku ya
Alhamis Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliwapa mamlaka wanajeshi
12,000 wa Umoja wa Mataifa waliopo nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati.(Awadh Ibrahim)
No comments:
Post a Comment