TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 01.04.2014.
- BIBI WA MIAKA 68 AUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA KWA TUHUMA ZA KISHIRIKINA.
- MZEE WA MIAKA 62 AFARIKI DUNIA BAADA YA KUZIDIWA NA MAJI YA MTO SAZA.
- MTOTO WA MIAKA 02 AMEKUTWA AMEKUFA MAJI BAADA YA KUTUMBUKIA NDANI YA KISIMA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
BIBI
WA MIAKA 68 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BELTA SANZIA MKAZI WA MAWENI
AMEUAWA KWA KUKATWA NA KITU KINACHODHANIWA KUWA SHOKA KICHWANI, MKONO WA
KULIA NA KUTOBOLEWA SEHEMU ZA UBAVU WA KUSHOTO NA MTU/WATU
WASIOFAHAMIKA.
TUKIO
HILO LA KUSITIKISHA LIMETOKEA MAJIRA YA USIKU WA KUAMKIA TAREHE
31.03.2014 HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAWENI, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI,
TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA MAUAJI
HAYO NI IMANI ZA KISHIRIKINA BAADA YA MAREHEMU KUTUHUMIWA KUWAROGA
WANAKIJIJI WENZAKE.
MAREHEMU ALIKUWA AKIISHI PEKE YAKE KATIKA NYUMBA YAKE. JUHUDI ZINAENDELEA KUWASAKA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHANA NA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA
KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MZEE
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LUCHAGULA MAENZEKA (62) MKAZI WA
KITONGOJI CHA KININGA AMEKUTWA AMEKUFA MAJI NDANI YA MTO SAZA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 31.03.2014 MAJIRA YA SAA 09:30 ASUBUHI HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA KININGA, KIJIJI NA KATA YA SAZA, TARAFA YA KWIMBA,
WILAYA YA CHUNYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA KIFO HICHO NI MAREHEMU
KUSHINDWA KUYAMUDU MAJI YA MTO HUO KUTOKANA NA ULEVI HALI ILIYOPELEKEA
KUSOMBWA NA MAJI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI WANAPOVUKA MITO HASA KIPINDI
HIKI CHA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KWANI NI HATARI. AIDHA ANATOA WITO
KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUNYWA POMBE KUPINDUKIA KWANI NI HATARI SI TU
KWA AFYA ZAO BALI HATA KWA MAISHA YAO.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MTOTO
MDOGO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JULIETA CHRISTIAN (02) MKAZI WA SAZA
AMEKUTWA AMEKUFA MAJI NDANI YA KISIMA KILICHOPO JIRANI NA NYUMBA
WANAYOISHI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 31.03.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI
KATIKA KITONGOJI CHA KATI, KIJIJI NA KATA YA SAZA, TARAFA YA KWIMBA,
WILAYA YA CHUNYA. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA MAREHEMU ALIBAKI PEKE YAKE
NYUMBANI BILA MWANGALIZI YEYOTE.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA
WATOTO WAO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA. AIDHA ANATOAN WITO
KWA JAMII KUFUNIKA VISIMA VILIVYOWAZI, KUFUKIA MADIBWI NA MASHIMO KWANI
NI HATARI KWA WATOTO WADOGO HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA
ZINAZOENDELEA KUNYESHA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
No comments:
Post a Comment