Pages

Saturday, April 5, 2014

DEREVA WA BASI LA PRINCES MURO MATATANI KUUA KWA KUGONGA MTEMBEA KWA MIGUU IRINGA

NA FRANK KIBIKI JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia dereva wa basi la abiria la PrinceS Muro, ambalo hufanya safari zake kati ya Mbeya na Dar es salaam, Said Mtatifikolo, kwa tuhuma za kumuua mtembea kwa miguu baada ya kumgonga.   Kaimu Kamanda wa jeshi hilo, Nyingesa alisema kuwa ajali hiyo, imetokea juzi jioni katika eneo la Viwengi wilayani Iringa.   Nyigesa alisema ajali hiyo ilitokea baada ya basi hilo lenye namba za usajili T 528 BVP, kumgonga na kumuua mtembea kwa miguu ambaye jina lake bado halijafahamika kutokana na mwili wake kuharibika.   Hata hivyo alidai kuwa upelelezi juu ya ajali hiyo unaendelea na kwamba, mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa  uchunguzi.
BOFYA HAPA LIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGII

No comments:

Post a Comment