Yakiwa
yamebaki mda mchache kabla ya mchezo wa pili wa hatua ya robo fainali ya
Champions league kati ya Chelsea dhidi ya PSG, Raisi wa klabu ya PSG
Nasser Al-Khelaifi ametoa ofa nzito kwa wachezaji wa klabu hiyo endapo
watafanikiwa kuitoa Chelsea leo hii.
PSG ambao waliifunga Chelsea 3-1 wiki
iliyopita jijini Paris wana nafasi ya kusonga mbele kutokana na ushindi
walionao mkononi lakini katika kuhakikisha timu yake inafanya vizuri
Al-Khelaifi ametoa ofa ya kiasi cha €450,000 ni zaidi ya billioni 1 kwa fedha
za madafu, kwa kila mchezaji wa PSG endapo klabu hiyo itafanikiwa kuingia nusu
fainali.Hatua inakuja siku chache baada ya kutoa ahadi ya €400,000 kwa kila mchezaji ikiwa tu watatetea kombe la ligue 1
No comments:
Post a Comment