Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, April 27, 2014

HUYU NDIO CAMERA MAN NAMBA MOJA KWA UBORA WA KAZI ZAKE NDANI YA BONGO MOVIE

Kabuti Onyango akiwa Location

Kabuti Onyango ndiyo jina la Kamera Man huyu mbunifu na mwenye viwango vya juu katika utengenezaji na kushoot Filamu ndani ya Tanzania.Mtandao wetu wa Dj sek blog ulipta nafasi ya kuongea na camera man huyu na ndipo tulipogundua kumbe jamaa ana kipaji na uwezo mkubwa,Kabuti alisema kwamba ana uzoefu wa miaka takribani 5 katika uchukuaji wa video za filamu akitumia camera yake ya kisasa aina ya panasonic.Kwanini tunasema Kabuti ndiye kamera man namba moja ndani ya bongo movie?ni kwamba jamaa amefanya zaidi ya filamu 5 ambazo zote zimeshawai kushika namba moja kwenye soko la filamu za kitanzania,Moja ya Filamu alizo shoot Kabuti ni Pusi na paku,Gumzo,Tikisa,Tom Boy na nyingie nyingii.Na Filamu zote hizo alizotoa zimeuza kwa wingi sana kwenye soko la filamu.


Unamjua Salma Jabu au maarufu Nisha basi huyu dada pia kapita kwenye mikono ya kamera man huyu mahiri kwani ameweza kufanya nae Filamu zaidi ya mbili ambazo ni Gumzo na Pusi na paku ambazo zilipelekea Nisha kushika namba moja kwenye mauzo ya Filamu sokoni.Pia  Kabuti amemsaidia sana msanii Nisha kwa vitu vingi sana kisanaa kwa ushauri na maelezo yakinifu yaliyopelekea mwanadada huyu kushika kwa sana ndani ya sanaa ya Bongo movie.
Na kwa sasa jamaa ameshoot Filamu kali inayokwenda kwa jina la Tom boy ambayo itatoka hivi karibuni

No comments:

Post a Comment