Pages

Wednesday, April 2, 2014

JE UNA WAZO LA BIASHARA? JIULIZE KWANZA, KWANINI UNATAKA KUANZA BIASHARA SASA?


Kama ndio kwanza unamaliza chuo na mazingira ni magumu kupata kazi. Inawezekana uko katika mazingira mazuri kuliko mtu ambaye hajaaenda shule kama yako. Je una mtazamo gani? Na umejipanga vipi? Ukweli unaotakiwa kujua ni kwamba wanafunzi wanaohitimu vyuo ni wengi kuliko kazi zilizopo.Changamoto ya ajira ni kubwa sana, inahitaji uwe mbunifu na mtu unaweza kupenya kwenye ushindani wa sasa kwenye ajira. 

Je mbadala wake ni nini?
Wakati mambo yanapoendelea kuwa magumu, hekima ya kawaida mtaani ni kusema usijague kazi , je una mbadala? Maisha yako mikononi mwako, unaweza kufanyishwa kazi sana, ukalipwa kidogo, au hata kuachishwa kazi na ukashindwa kupambana na maisha ya kila siku. Au fanya kazi kwa masaa unayotaka, kazi unayoipenda na kwa wateja unaowapenda na mshahara utakaochagua, je inawezekana? 

Mpango mbadala wa maisha yako ya baadaye.
Ukiweza kumiliki biashara yako, wewe ndio mtengeneza sheria za kazi ukiondoa zile za nchi zinazohusisha kazi ambazo unatakiwa kuzifuata. Inamaanisha kwamba kila kitu kitakuwa kikifanyika kwa maamuzi yako na vile unataka kifanyike bila kuvunja sheria za nchi. Hautaamka saa kumi na moja alfajiri ili uweze kuingia saa mbili asubuhi ofisini, utapangilia muda wako wa kazi kwa namna unavyotaka ila mafanikio na kushindwa yako mikononi mwako. 
Inawezekana unasema nitafanya nini? Je hali ya soko nitaiweza? Lakini ukiweza kuanza kufanya biashara sasa hivi, utafika mbali usipopoteza dira.
Vilevile kama utapata kazi na una muda wa ziada unaweza kuanzisha biashara usiwe kama watu wengine ni waoga wa kufanya biashara wanasubiri tu mwishowa mwezi wafanye kazi au wasifanye kazi. Je jielize kama ungemwajiri mtu afanye kazi kama unayofanya hapo we ungemlipa kiasi gani? 

Kila mtu anaweza kufanya biashara
Kufanya biashara kunahitaji malengo na ujuzi wa kujua soko linasemaje na linahitaji nini na wewe unaweza kupeleka nini sokoni kulingana na uhitaji wake. Usipeleke sokoni kitu ambacho huna uhakika wa kinachohitajika. Fanya uchunguzi wa bei na watu vinapatikana na kwa gharama gani? Je wewe unaweza kutoa kitu kizuri na bora zaidi kuliko kilichopo sokoni? Na usifikiri kila anayefanya biashara atafanikiwa, inategemea unaweza vipi kufanya biashara, kama huwezi usiingie wewe endelea kuajiriwa tu. 

Hatua ya Kwanza: Ondoa fikra potofu kichwani mwako
Ukiondoa fikra potofu kwenye mawazo yako itakuwa rahisi kupata mawazo ya kimaendeleo zaidi. Je unajua nini ukisikia mtu anafanya biashara? Na ukweli wa mambo kwenye biashara ni nini? Watu wa mtaani wanasemaje kuhusu biashara? Je wewe unaweza kufanya biashara?

Hatua ya Pili: Tafuta “kitu unachokipenda”
Utakapojua kitu unachopenda kufanya na je kinaweza kuwa biashara? Uwezekano wa kufanikiwa zaidi ni mkubwa kuliko kurukia mambo. 

Hatua ya Tatu: Pangilia hicho kitu unachokipenda
Kitu unachokipenda kiweke kwenye mpango wa biashara, tafuta gharama zake na ukianza kuuza ni nini bei yake? Je utawalenga watu gani? Usipojua unawalenga watu gani, biashara yako haitaweza kusimama. 

Hatua ya Nne: Tawala Soko lako
Wahusishe wateja wako na Bidhaa yako. Inamaanisha kwenda zaidi ya watu wengine wanachokifanya kwenye biashara, uwe mbunifu wa kuifanya bidhaa yako ijulikane na kukua kwenye soko. 

Hatua ya Tano: Jenga kijiji chako kibiashara
Unahitaji kuisaidia biashara yako ikue, hivyo tengeneza mazingira ambayo biashara yako itakapotawala ili kusaidia kuikuza hiyo biashara. Kumbuka mafanikio hayaji ghafla ghafla, utahitaji kufanya kazi sana, kuwa mbunifu, mvumilivu na mwenye stamina ya kuhimili vishindo kwenye soko. 




 


No comments:

Post a Comment