MAANDALIZI ya ujenzi
wa kijiji cha michezo kitakachojulikana kama Jakaya Kikwete Sports Village
yanaendelea vizuri, ambako tayari Ikulu, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na
Wizara ya Michezo wametoa baraka kijengwe mjini Dodoma.
Akizungumza
na Tanzania Daima, Mratibu wa ujenzi wa kituo hicho, Wilhelm
Gidabuday, alisema ujenzi wa kituo hicho kikubwa na cha kwanza nchini, tayari
maandalizi yake yameshafikia pazuri na Ikulu ya Tanzania kupitia ofisi ya
Katibu wa Rais, imeshawapa baraka ya kutumia jina la Rais katika kituo hicho.
Gidabuday alisema,
wiki iliyopita walikutana na Katibu wa Rais, ambako waliwasilisha maombi yao na
kukubaliwa na kwamba, kuanzia sasa kituo hicho ambacho ujenzi wake utasaidia
kuinua vipaji vya michezo yote hapa nchini, kitafahamika kama kituo cha michezo
cha Jakaya Kikwete (Jakaya Kikwete Sports Village).
“Nidokeze
tu kuwa, mipango yote inakwenda sawa, tumeshafikisha ujumbe wetu Ikulu na
imekubalika, awali tulipanga kituo chetu tukiite John Steven Akhwari Sports
Village, lakini baada ya kukaa na Mzee Akhwari, kwa pamoja tuliridhia kituo
hiki kitumike kama sehemu ya kumpa heshima
Rais wetu, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, hivyo kitafahamika kama Jakaya Kikwete Sports Village,” alisema Gidabuday.
Rais wetu, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, hivyo kitafahamika kama Jakaya Kikwete Sports Village,” alisema Gidabuday.
Gidabuday ambaye pia
anaratibu mbio za Kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha Sokoine, Sokoine Mini
Marathon, pamoja na matembezi ya amani kutoka Ujiji – Kigoma mpaka Dar es
Salaam, alisema wamepanga kutumia shughuli zote mbili kuwafahamisha wananchi
kuhusu umuhimu wa ujenzi wa kituo hicho katika maendeleo ya sekta ya michezo na
utamaduni hapa nchini.
Wakati huo huo,
waandaaji wa msimu wa pili wa Sokoine Mini Marathon, zitakazofanyika Kijiji cha
Monduli Juu, wametangaza rasmi sehemu ambako fomu za ushiriki wa mbio hizo
zitapatikana.
Akizungumza na
waandishi wa habari, Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday, alisema, fomu za
ushiriki wa mbio hizo kwa mwaka huu zitapatikana wilayani Monduli, katika
Kijiji cha Monduli Juu.
No comments:
Post a Comment