Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, April 14, 2014

LIVERPOOL WANUSA NUSA HARUFU YA UBINGWA NI BAADA YA KUITANDIKA MANCHESTER CITY GOLI 3 KWA 2


NAHODHA wa Liverpool, Steven Gerrard ameanfgusha kilio cha furaha baada ya timu yake kuukaribia ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza baada ya miaka 24 kufuatia ushindi wa mabao 3-2 dhidinya mahasimu wao katika mbio za taji, Manchester City jioni hii Uwanja wa Anfield


Bao la furaha la Liverpool limefungwa na Philippe Coutinho dakika 12 kabla ya filimbi ya mwisho, baada ya mabao mengine ya timu hiyo kufungwa kipindi cha kwanza na Raheem Sterling dakika ya sita na Martin Skrtel dakika ya 26.
Lakini City ilipigana na kusawazisha hadi kuwa 2-2 kwa mabao ya kipindi cha ya David Silva dakika ya 75 na Glen Johnson aliyejifunga dakika ya 63, lakini makosa ya Nahodha wa City, Vincent Kompany yalimpa Coutinho nafasi ya kaumua mshindi wa mechi.
Baada ya mechi, Nahodha wa Wekundu hao, Gerrard alionekana kumwaga machozi kabla ya kuwakumbatia wachezaji wenzake. Liverpool sasa inatimiza pointi 77 baada ya kucheza mechi 34 na kuendelea kujinafasi kileleni, wakati City inabaki na pointi zake 70 za mechi 32 na kuendelea kubaki nafasi ya tatu. Chelsea yenye pointi 75 za mechi 34 ni ya pili. 
Shujaa: Philippe Coutinho akishangilia baada ya kuifungia bao la ushindi Liverpool dhidi ya Manchester City leo

No comments:

Post a Comment