Pages

Monday, April 7, 2014

MAAJABU YAFANYIKA LIGI KUU TANZANIA JIONEE HAPA

KAVUMBAGO NA KIPA SHABANI DIHILE WAKIWANIWA MPIRA PICHA ZOTE na mzuka wa fungo
KIPA SHABANI DIHILE NA KAVUMBAGO WAKIWANIA MPIRA GOLINI MWA JKT RUVU

WACHEZAJI WA YANGA WAKISHANGILIA BAO LILILOFUNGWA NA MRISHO NGASSA KATI MCHEZO WA LIHI KUU YA VODACOM YANGA ILIFUNGA JKT RUVU BAO 5-1


BEKI WA JKT RUVU JAMALI MACHELANGA AKIMBANA NGASSA KATIKA PAMBANOI LA LIGI KUU

 TIMU zilizopo katika hatari ya kushuka daraja, Oljoro JKT, Mgambo JKT na Rhino Rangers zimeibuka na ushindi katika mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara. Ushindi wa timu hizo umezidi kufanya kinyang'anyiro cha timu za kutaka kushuka daraja kuzidi kunoga kwani hakuna aliyena uhakika mpaka sasa wa kushuka au kubakia katika ligi hiyo mpaka sasa ligi ikiwa kwenye raundi ya 24. Mgambo ikiwa kwenye uwanja wa Mkwakwani ilipepetana na Coastal Union na kupata ushindi wa mabao 2-0. Mabao ya washindi walitoka kuifumua Yanga wiki iliyopita yaliwekwa kimiani na Peter Malianzi, Boli Ajali 

na 'Wazee wa Oman' wakishindwa kufurukuta kwa maafande hao ambao wamejiweka katika nafasi nzuri ya kupona kuteremka Ligi Daraja la Kwanza.
Katika mechi nyingine iliyochezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha wenyeji waliopo nafasi ya pili toka mkiani wakipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya maafande wa Prisons-Mbeya, huku Rhino inayoburuza mkia ikishinda bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Ligi hiyo itaendelea tena siku ya Jumatano kwa mechi ambazo zinaweza kuamua hatma ya ubingwa baona ya Yanga na Azam, wakati timu hizo zitakapokuwa viwanja viwili tofauti.
Yanga itakuwa uwanja wa Taifa kupepetana na Kagera Sugar wakati Azam itawafuata Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Mabatini-Mlandizi.
Azam inaoongoza msimamo kwa pointi 53 na Yanga iliyoifumua JKT Ruvu jioni hii mabao 5-1 inafuatia ikiwa na pointi 49 na Mbeya inafuata na pointi 46 katika nafasi ya tatu, kisha Simba yenye pointi 37.

No comments:

Post a Comment