skip to main |
skip to sidebar
MADUKA YA WATANZANIA SOUTH AFRICA YACHOMWA MOTO-WADAIWA KUUZA UNGA
Afrika Kusini ni nchi yenye uchumi
mkubwa Afrika ambao umevutia Waafrika wengi kukimbilia huko kwa ajili ya
kufanya kazi kama za Udereva, uuzaji mafuta kwenye vituo vya mafuta
pamoja na kazi nyingine mbalimbali.
Taarifa kutoka kwenye mji wa Pretoria ni
kwamba Watanzania ambao wanamiliki na kufanya biashara mbalimbali
zikiwemo za Maduka na wale wanaomiliki hoteli, wamevamiwa wakiwa kwenye
mali zao na kufanyiwa uharibifu na nyingine kuchomwa moto.
Ni kundi la watu ambalo linaendeleza
uvamizi huu ambapo linawashutumu Watanzania hawa kuhusika na biashara ya
dawa za kulevya, yani kwa ufupi Watanzania wanasema hata kama kweli
wangekua wanafanya hii biashara, walio na mamlaka ya kuwavamia ni Polisi
na sio hao raia.
Inaaminika kundi hili lina sehemu kubwa
ya madereva Taxi wazawa wa nchi hiyo ambao wamekua wakiumizwa na
jitihada za raia wa kigeni wa Nigeria na Watanzania ambao wamejazana
kwenye mtaa wao wakimiliki maduka mbalimbali yakiwemo ya nguo pamoja na
hoteli.
Tayari balozi wa Tanzania amekutana na
Watanzania hao na kuahidi kulifatilia ambapo ni Watanzania watano
wamejeruhiwa wakiwemo watatu ambao bado wako hospitali na mmoja wao
kavunjika mkono, mmoja kapigwa kichwani.
Kabla ya Watanzania wengine kuwahi
kufunga maduka yao, maduka matatu ya Watanzania pamoja na hoteli mbili
zinazomilikiwa na Watanzania zilivamiwa na wakachuchukuliwa simu na watu
kupigwa ambapo polisi walipokuja hakuna chochote kilichofanyika zaidi
ya maelezo.
Picha hizi zote zilipigwa na Mtanzania akiwa anakimbia baada ya kufanikiwa kufunga duka lake.
No comments:
Post a Comment