KOCHA
Mkuu wa Mashetani wekundu, Manchester United, David Moyes amemuambia
mwamuzi wa Hispania, Carlos Carballo kutoa maamuzi sahihi katika mchezo
wao dhidi ya mabingwa wa Ulaya na Bundesliga, Bayern Munich kutokana na
tabia ya wachezaji wa timu hiyo kujiangusha.
Man
United inakabilina na Bayern usiku wa leo uwanja wa Old Trafford
katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali, Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Bayern
inapewa nafasi kubwa ya kushinda, lakini timu hiyo ya kocha Pep
Guardiola ilishutumiwa baada ya kuitoa Arsenal katika raundi iliyopita,
huku kocha wa washika bunduki wa London, Arsene Wenger akimlaumu Arjen
Robben kuwa ni hodari wa kujirusha kujiangusha.
Moyes
alisema: “Tunawaamini marefa watafanya uamuzi sahihi. Kujirusha ni moja
ya vitu vibaya vya kufanyia kazi. Ningependa kutahadharisha juu ya
hilo, lakini nisingependa kumlenga mchezaji binafsi,”.
Angalizo
la tahadhari: Kocha wa Manchester United, David Moyes anatumai refa
Carlos Velasco Carballo atwaadhibu wachezaji wa kujiangusha,NA BARAKA MPENJA
BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KUSISIMUA
No comments:
Post a Comment