Pages

Tuesday, April 1, 2014

News: Frank Domayo asajiliwa Simba SC; kutua Msimbazi msimu ujao

Shaffih Dauda: Siku chache baada ya kugundulika mkataba wake ndani ya klabu ya Yanga unamalizika mwishoni mwa msimu huu, klabu ya Simba imefanikiwa kumsajili rasmi kiungo Frank Domayo kutoka kwa mahasimu wao wa Wajangwani.
Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba Domayo anakaribia kumaliza mkataba wake na Yanga, na Simba walipogundua hilo wakazungumza haraka na mchezaji huyo na kufanikiwa kumpa mkataba mzuri huku Domayo akilamba millioni 40 kama fedha ya usajili.

Mchezaji huyo atajiunga na Simba baada ya ligi kumalizika. Simba wamejipanga kisawasawa kujiimarisha msimu ujao baada ya kufanya vibaya msimu huu - na usajili wa Domayo ni mwanzo tu wa kuimarisha timu yao.




 

No comments:

Post a Comment