Pages

Wednesday, April 23, 2014

PICHA ZA REAL MADRID WAKIJIANDAA NA MCHEZO WA LEO DHIDI YA BAYERN

Cristiano Ronaldo anatarajia kurudia dimbali kuitumikia Real Madrid leo kwenye mchezo wa awali wa nusu fainali ya Champions League dhidi ya Bayern Munich katika uwanja wa Santiago Bernabeu.
Kocha wa Madrid Carlo Ancelotti amesema atafanya maamuzi juu ya mchezaji huyo mwenye miaka 29 ambaye alikosa michezo minne ya mwisho ya klabu hiyo ukiwepo mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalme ambapo Madrid waliishinda Barcelona 2-1.
Naye Boss wa Bayern Munich Pep Guardiola hajawahi kupoteza hata mchezo mmoja katika michezo sita aliyocheza na Real Madrid katika dimba la Bernabeu.
Bayern Munich imeichapa Real Madrid mara nne katika michezo mitano ya nusu fainali ya European Cup ambapo timu hizo zimekutana.
Real inajivunia rekodi yao ya kutwaa taji la Champions League mara tisa lakini inalisaka taji hilo kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 12.

No comments:

Post a Comment