Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, April 12, 2014

RUAHA IMETAPIKA, TUNASUBIRI KISINGIZIO TANESCO!


20140403_124437_9eed1.jpg

Mto Ruaha Mdogo unaokatiza mpaka kwenye Manispaa ya Iringa 'umetapika', au umefurika katika maeneo mengi. Mashamba ya pembezoni mwa mto huo, yamefunikwa na
maji na wakulima wengi wanalia.
Wenyeji wa mkoa wa Iringa wanasema kwamba, mafuriko ya mwaka huu hayajawahi kutokea katika miaka 10 iliyopita tangu walipoyashuhudia mafuriko ya mwaka 1998 wakati wa Mvua za El Nino.
Mto huo ndio unaoungana na Ruaha Mkuu kumwaga maji katika Bwawa la Mtera na hatimaye kwenye Mto Kilombero kuelekea Rufiji.
Hata Bwawa la Mtera, linalotumika kwa shughuli mbalimbali za uchumi kama uvuvi na hata uzalishaji wa umeme, nalo lina maji ya kutosha. Sijui mwaka huu Tanesco watatuambiaje tutakapoona giza!CHANZO MJENGWA


No comments:

Post a Comment