“Sitakwenda kumuona Kikwete, bali ninajua kwamba tukishindwa kuipata Tanganyika kwenye Bunge hili nitakwenda mahakama za kimataifa,” alisema Mtikila ambaye amekuwa akihubiri Utanganyika tangu nchi ilipoingia kwenye siasa za vyama vingi mwanzoni mwa miaka ya tisini.
Alisema kwa sasa anasubiri kumaliza majadiliano
juu ya sura ya kwanza na ya sita ya rasimu ya katiba kuona mwelekeo na
suala la muundo wa Muungano kuwa wa serikali tatu litakwamishwa,
ataondoka Dodoma na kurejea Dar es Salaam kuandaa kesi.
Hoja kubwa katika mchakato wa kutunga Katiba mpya
iko kwenye muundo wa Muungano baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba
kuwasilisha rasimu inayoonyesha kuwa wengine wanataka muundo wa Muungano
wa serikali tatu, jambo ambalo linaonekana kupingwa na wajumbe kutoka
chama tawala cha CCM.
Bunge hilo linaundwa na wabunge wote wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano, wawakilishi wa Baraza la wawakilishi wa Zanzibar na
wawakilishi wa makundi mbalimbali wapatao 201 ambao walitangazwa na
Rais Kikwete.
Lakini Mchungaji Mtikila anapingana na muundo wa Bunge la Katiba.
“Nitakwenda mahakamani kupinga sheria yote ya
Mabadiliko ya Katiba kwani waliopaswa kushiriki Bunge la Katiba ni
wajumbe waliochaguliwa na wananchi kwa ajili ya Bunge la Katiba, na siyo
hawa wabunge na wengine wa kuteuliwa,” alisema.
Hoja ya Mtikila
Pamoja na mambo mengine katika hoja yake, Mtikila
analalamika kuwa amezuiwa kuchangia katika Bunge hilo baada ya
kuandikiwa barua na Ofisi ya Bunge.
Hata hivyo, katibu wa Bunge la Katiba, Yahya Khamis Hamad alisema: “Hili kwangu ni jipya na sidhani kuwa linawezekana.”
Mtikila alisisitiza kuwa alipewa barua hiyo
Jumatano iliyopita ikiwa ni majibu ya barua yake aliyoiandika kwa ofisi
hiyo wiki iliyopita.
“Nilianza kuhisi baada ya kuona ninanyimwa
kuchangia; nikaandika barua kuomba maelezo kwa nini ninakosa nafasi ya
kuchangia bungeni,” alisema na kuongeza:
“Lakini juzi nilipokea barua kutoka kwa katibu wa
Bunge ikinikataza kuchangia tena bungeni kutokana na kauli zangu za
kukosoa mchakato.”chanzo Mwanainchi
No comments:
Post a Comment