Pages

Tuesday, April 1, 2014

TAARIFA YA MSIBA: MAMA MZAZI WA SAID MDOE WA SALUTI5 AFARIKI DUNIA

MAMA mzazi wa mmiliki wa mtandao wa Saluti5,
Said Mode - Bi Desta Mohamed - amefariki ghafla Jumatatu ya tarehe 31/3/2014 saa 1 za jioni.

 Alipata homa kali Jumapili mchana, akapelekwa hospitali (IMTU) akapata matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani. Hali yake haikuwa mbaya wala ya kutia mashaka.

 Jumatatu akaamka vizuri na akashinda vizuri hadi saa 12 za jioni hali ipoanza kubadilika tena. Akafariki akiwa njiani kupelekwa hospitali. Msiba uko Dar es Salaam, Mbezi Beach Old Bagamoyo Road kituo cha Zena Kawawa.

Mazishi yatafanyika Jumanne 1/4/2014 saa 10 alasiri kwenye makaburi ya Mbezi Beach (New Bagamoyo Road) mbele kidogo ya  Masana Hospital.



INNA
LILLAHI WAINNA ILAYHI RRAAJIUN.

No comments:

Post a Comment