Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kinatoa tamko la awali kwa
umma kuhusu ukiukwaji mkubwa wa taratibu, kanuni na sheria zinazosimamia
uchaguzi, zilizofanyika kwenye mchakato wa uchaguzi mdogo wa ubunge
Jimbo la Chalinze, ambao umehitimishwa Aprili 6, mwaka huu, kwa wapiga
kura wa jimbo hili kupiga kura;
Ukiukwaji huo ni kama ifuatavyo;
- Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuongeza wapiga kura wapya kinyume cha sheria
“Kwa madhumuni ya kifungu hiki, Tume itapitia upya daftari la kudumu la
taifa la wapiga kura mara mbili kati ya kipindi kinachoanza mara baada
ya uchaguzi mkuu na tarehe inayofuatia siku ya uteuzi,”
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekiuka kifungu hiki cha sheria kwa kufanya
kile wanachoita wao ni ‘uhakiki wa mwaka 2014’ wa daftari ambao wanadai
lengo lake lilikuwa ni kupunguza idadi ya wapiga kura waliokufa au
kuhama au kuandikishwa mara mbili, lakini badala ya
wapiga kura kupungua, uhakiki huo uliofanywa na tume bila kushirikisha
wala kuwataarifu wananchi wa Jimbo la Chalinze, umeongeza idadi ya
wapiga kura wapya katika jimbo hili kwenye uchaguzi huu mdogo.
Vile vile, kutokana na kitendo hicho cha NEC kuongeza idadi ya wapiga kura wapya kwenye daftari kimesababisha kuongezeka kwa vituo vya kupigia kura tofauti na ilivyokuwa mwaka 2010, ambapo Jimbo la Chalinze lilikuw ana jumla ya vituo 286 na sasa vimekuwa 288.
- Kutangaza matokeo kinyume cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi
Kitendo hicho kilikuwa kinyume na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, kifungu 80(3), kinachosema;
“Baada ya taarifa zote za matokeo na masanduku ya kura yaliyo na karatasi za kura za uchaguzi wa bunge kupokelewa kutoka vituo vya kupigia kura katika jimbo, Msimamizi wa Uchaguzi, baada ya kuamua uhalali wa kura zozote zenye mgogoro na kabla ya kujumlisha kura hizo, atatangaza kwa sauti matokeo ya kila kituo cha kupigia kura katika jimbo kimoja baada ya kingine.”
Badala yake, Msimamizi wa Uchaguzi alitangaza matokeo ya jumla kwa kila kata, bila kufanyika kwa majumuisho kama sheria inavyotaka, jambo ambalo linapelekea matokeo yaliyotangazwa kutokuwa halali kisheria, huku yakitofautiana na matokeo tuliyonayo kwa mujibu wa fomu za matokeo.
- Matumizi ya rasilimali za umma kuibeba CCM na mgombea wake
Kuna mifano mingi katika suala hili; upo ushahidi unaonesha kuwa Rais Jakaya Kikwete alikuwa akifika jimboni hapa kwa kutumia magari ya serikali na watumishi wa umma, ambapo alihusika kufanya kampeni za ‘mtu kwa mtu’.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Ally Mohamed Shein, ambaye alikuja Chalinze kwenye mkutano wa ufungaji wa kampeni za chama chake huko Miono, naye alitumia rasilimali za umma, k.m; magari na watumishi (wakiwemo kutoka vyombo vya ulinzi na usalama), waliokuwa kwenye msafara wake, kufanya kampeni za chama cha siasa, kushawishi na kuelekeza wapiga kura, kinyume kabisa na sheria na taratibu za uchaguzi.
Mama Salma Kikwete ambaye ni kiongozi mwandamizi wa CCM, kwa muda takriban wote wa kampeni alikuwa akitumia rasilimali za umma kama vile magari (yaliyokuwa na namba za ikulu) na watumishi, kufanya kampeni za kumnadi mgombea wa chama chake.
- CCM kufanya kampeni siku ya uchaguzi
Kitendo hicho cha Rais Kikwete ambacho kililenga kufanya kampeni, kushawishi na kuelekeza wapiga kura, ni kinyume na Sheria ya Uchaguzi, kifungu cha 104 (1), ambacho kinasema;
“Hakuna mtu atakayefanya mkutano siku ya kupiga kura au; ndani ya jengo lolote ambamo upigaji kura katika uchaguzi unaendelea, au mahali popote ndani ya eneo la mita 200 ya jengo hilo…kuonesha upendeleo au nembo nyingine inayoonesha kuunga mkono mgombea fulani katika uchaguzi.”
Kifungu cha 104 (2) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, kinasema;
“Mtu yeyote atakwenda kinyume na kifungu hiki, atakuwa amefanya kosa…”
- Vishawishi vya rushwa kwa ajili ya kujitoa
Imetolewa leo Bagamoyo, Aprili 7, 2014 na;
John Mrema
Mkuu wa Operesheni ya Uchaguzi Mdogo-Chalinze
BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGIIIII
No comments:
Post a Comment