Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu faida za Mtambo Maalum wa Kusimamia Mawasiliano na Udhibiti wa Mapato yatokanayo na Simu unaojulikana kama Telecommunication Traffic Monitoring System (TTMS). Mtambo huo unaweza kutambua mawasiliano ya udanganyifu katika mitandao na namba za ulaghai zinazotumika kwenye mawasiliano ya kimataifa kinyume cha sheria. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi.
Naibu Mkurugenzi anayehusika na usimamizi wa Mtambo Maalum wa Kusimamia Mawasiliano na Udhibiti wa Mapato ya Simu (TTMS) kutoka TCRA, Mhandisi Sunday Richard akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jinsi mtambo huo unavyofanya kazi ya kudhibiti udanganyifu katika mitandao ya simu za kimataifa zinazoingia hapa nchinI
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika jijini Dar es Salaam. Lengo la Mkutano huo ni kuelezea mtambo wa TTMS unavyodhibiti udanganyifu katika mitandao ya simu za kimataifa.
PICHA ZOTE NA FATMA SALUM- MAELEZO
No comments:
Post a Comment