WANANCHI wenye hasira kali wakazi wa mtaa wa Mtwivila D katika Manispaa ya Iringa wamemuua mtuhumiwa mwingine wa ujambazi aliyetambulika kwa jina la Ayubu Mhema (31) msukuma mkokoteni mkazi wa Wangama mkoani Njombe kwa tuhuma za wizi wa mali za wananchi wa eneo hiloTukio hilo lilitokea leo majira ya saa 3 asubuhi baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa akiwa na nguo zilizojaa ngunia moja ambazo aliziiba katika nyumba ya mkazi mmoja wa eneo hilo baada ya kuvunja mlang
Hapa mwili wa mtuhumiwa huyo ukishushwa kwa ajili ya kuhifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa |
Mtuhumiwa wa wizi Ayubu Mhema akiwa amelala hoi |
Wakizungumza na mwandishi wa habari hii pasipo kutaja majina yao wananchi hao walisema kuwa kumekuwepo na matukio endelevu ya wizi katika eneo hilo na mbali ya wezi hao kukamatwa na kufikishwa polisi ila bado wamekuwa wakiachiwa huru jambo ambalo limeongeza wimbi la wizi katika eneo hilo.
Hata hivyo walisema mtuhumiwa huyo Mhema amepatwa kukamatwa eneo hilo zaidi ya mara nne akiwa na wenzake ila mbali ya kupewa kichapo bado amekuwa akirudia kuiba .
Mbali ya kulalamikia matukio hayo ya wizi yanayoendelea katika eneo hilo bado waliwatuhumu viongozi wa serikali ya mtaa kwa kushindwa kuitisha mkutano wa dharula kwa ajili ya wananchi kupiga kura ya siri kwa lengo la kuwataja watu ambao wamekuwa wakijihusisha na mtandao wa wizi na wale wanaofunga mtandao huo ambao baadhi yao wanadaiwa ni viongozi wa mtaa huo.
" Tumekuwa tukiomba kufanyika kwa mkutano na kila wiki mtendaji na mwenyekiti wamekuwa wakisogeza mbele mkutano huo huku wananchi tukiendelea kunyanyasika na mtandao huo wa wezi ....ila tunasubiri kwa mara nyingine mkutano wa April 27 kama walivyotangaza na iwapo watashindwa tutapambana na viongozi hawa kwa kumkataa mtendaji wa mtaa na kata pamoja na wajumbe wake wote "
Kwani walisema katika mkutano wa mwisho uliofanyika mwezi uliopita mbele ya diwani wa kata ya Mtwivila Vitus Mushi wananchi kwa kauli moja waliomba mkutano huo ila viongozi hao wamekuwa wakimpuuza hadi diwani wao kwa kushindwa kusikiliza maombi ya wananchi .
Pia walisema orodha kamli ya majina ya mtandao huo wa wezi ilitajwa na mtuhumiwa huyo Mhema kabla ya kufariki ambapo mtandao huo upo stendi ya Mlandege ,stendi kuu , Ilala kwa Mlyuka pamoja na Kihesa ambako ndiko yupo mmiliki wa mtandao huo ambapo majina yao yamehifadhiwa .
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia polisi wakifika eneo hilo wakiwa na mabomu ya machozi kwa ajili ya kumuokoa mtuhumiwa huyo na kumchukua kumkimbiza Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kabla ya kufariki dunia njiani .
Ndani ya wiki hii moja wananchi hao wa mtaa wa Mtwivila D wamewatesa hadi kufa watu wawili kwa tuhuma za wizi ambapo jeshi la polisi limewaonya wananchi hao kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi dhidi ya watuhumiwa wa wizi na kuwa kufanya hivyo ni kosa na ni kinyume na haki za binadamu.Chanzo:matukiodaima.com
BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGII
BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGII
No comments:
Post a Comment