CHACHA Makenge (38) aliyeripotiwa awali kuishi ndani ya handaki katika
eneo la pori la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani, amepatwa
na balaa jipya baada ya makazi yake kuvamiwa na askari, kukamatwa na
mwishowe kupelekwa Muhimbili kitengo cha wagonjwa wa akili kwa ajili ya
matibabu.
Kana kwamba haitoshi, Makenge ambaye aliwahi kuishi katika handaki hilo
kwa muda wa miaka mitano, alipotoka, alikuta makazi yake hayo yakiwa
yamechomwa moto na vitu vyake vyote kuchukuliwa.
Akizungumza na gazeti hili, kijana huyo alikiri kutokewa na mambo
hayo na kulalamika kuwa kitendo alichofanyiwa, kimempotezea mwelekeo wa
maisha yake kwani hana tena sehemu ya kwenda kwa kuwa hakujiandaa.
Alisema alipokamatwa alipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa
kudhaniwa kuwa ni mgonjwa wa akili, lakini alipingana na madai hayo,
licha ya kuwa aliishi kwa siku 36 hospitalini hapo kabla ya kuruhusiwa
kuondoka.
Mmoja wa maofisa wa ulinzi wanaolinda chuoni hapo, Mussa Nakuwa
aliyeendesha oparesheni ya kumkamata kijana huyo, alisema vifaa vyake
vyote vilipelekwa Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilaya ya Kinondoni kwa ajili
ya kuhifadhiwa na anaweza kwenda kuvichukua wakati wowote.
Habari zingine kuhusiana na mtu huyo zinadai amechimba mahandaki mengine kadhaa ya siri ambayo anayatumia kwa ajili ya kulala.
BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGIII
BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGIII
No comments:
Post a Comment