skip to main |
skip to sidebar
Wakazi wa kijiji cha Ng’ong’ona mkoani Dodoma wanakabiliwa na tatizo la maji hali inayopelekea kufuata huduma ya maji vijiji vya jirani.
Akizungumza na Dodoma fm mwenyekiti wa kijiji cha ng’ong’ona bwana
Venansi Kisumuni amethibitisha kuwepo kwa tatizo hilo na kukiri
kuwa maji ni tatizo kubwa hivyo wanalazimika kutumia maji ya korongoni
kwa matumizi ya nyumbani.
Nae bi Suzani matonya mkazi wa ngogona amesema kuwa amekuwa
akiteseka tangu utoto mpaka leo hajafanikiwa kupata maji mbali na
kutozwa michango mbali mbali kwa ajili ya huduma hiyo hivyo kuiomba
selikali iwasaidie kupata huduma ya maji.
Bwana venance amehitimisha kwa kusema kuwa kwa sasa wanalazimika
kununua maji kwa sh mia tatu hadi miato kutoka kwenye makaro hali inayo
wawia
vigumu kulingana na hali ya uchumi.Na Dodoma Fm
No comments:
Post a Comment