waziri
Mkuu Mizengo Pinda akitoa pile kwa waombolezaji kabla ya kutoa heshima
za mwisho kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Moshi
Chang’a, nyumbani kwa Marehemu Mbagala Kibonde Maji jijini Dar es salaam
Aprili 22, 2014. Kushoto ni mkewe Tunu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu na Mkewe Tunu
(kulia) wakitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya
Kalambo mkoani Rukwa, Moshi Chang’a, nyumbani kwa Marehemu Mbagala
Kibonde Maji jijini Dar es salaam Aprili 22, 2014. Kushoto ni mkewe
Tunu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Mizengo
Pinda ameongoza viongozi kadhaa na baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Dar es
Salaam kuuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Bw. Moshi
Chang’a ambaye alifariki dunia Aprili 20, 2014 kwenye Hospitali ya Taifa
Muhimbili ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Shughuli
ya kuuaga rasmi mwili wa marehemu Chang’a kwa wakazi wa mji wa Dar es
Salaam ilifanyika leo mchana (Jumanne, Aprili 22, 2014) nyumbani kwake
Mbagala, Kibonde Maji, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mwili wake
utasafirishwa leo jioni kwenda Kihesa, mkoani Iringa kwa mazishi.
Akizungumza
na waombolezaji hao kabla ya kutoa heshima za mwisho, Waziri Mkuu Pinda
alisema amemfahamu Bw. Chang’a kwa muda mrefu kwa sababu sehemu kubwa
ya utumishi wake ameifanya akiwa Serikalini.
“Ninyi
mlimfahamu Bw. Chang’a kivingine lakini mimi nilimfahamu kwa namna ya
tofauti kutokana na jinsi alivyokuwa msaada mkubwa kwa Serikali kila
tulipokuwa tukipata shida ama migogoro ya kiuongozi.”
“Kama
TAMISEMI, tumemtumia sana kusawazisha mambo kwa sababu Mungu alimjalia
kipaji cha pekee ambacho ni ucheshi… hata jambo lingekuwa gumu vipi,
huyu Bwana alijua kufikisha ujumbe bila kumuudhi mhusika kutokana na
maneno yake,” alisema Waziri Mkuu.
Alitumia fursa hiyo kufikisha salamu za rambirambi kwa wafiwa kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye yuko safarini kikazi.
Vilevile,
aliwataka wanafamilia ambao wamebaki bila mama wala baba, wawe na umoja
na mshikamano na kuahidi kuwa Serikali itawasaidia watoto wa marehemu
wakamilishe malengo ya elimu yao kama ambavyo baba yao alikuwa amepanga.
Marehemu
Chang’a anatarajiwa kuzikwa kesho (Jumatato, Aprili 23, 2014) huko
Kihesa, Manispaa ya Iringa ambapo Serikali itawasilishwa na Waziri wa
Nchi (OWM-TAMISEMI), Bibi Hawa Ghasia. Marehemu ameacha watoto watano,
wa kike watatu na wa kiume wawili.
No comments:
Post a Comment