Pages

Saturday, April 26, 2014

WILAYA MPYA 2 KUUNDWA MKOA WA DAR ONA NI WAPI NA WAPI

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said Mecky Sadick.
Mkuu wa Mkoa wa DarEs Salaam Said Mecky Sadick.
Wilaya mbili zinatarajiwa kuongezwa na kufanya idadi ya wilaya kuwa tano katika jiji la Dar Es Salaam. Wilaya hizo ni Kigamboni na Ubungo.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said Mecky Sadick  wakati wa kuhitimisha kikao na baraza la Mashauri jijini Dar Es Salaam siku ya Jumanne ambapo wilaya ya Kigamboni itagawanywa na kuwa na majimbo mawili ya Mbagala na Kigamboni.
“Mapendekezo hayo yatafikishwa kwenye serikali kuu na uamuzi wake utatolewa mwezi ujao’, alisema Mkuu wa Mkoa , ambaye alikuwa mwenyekiti wa baraza hilo, lililokuwa likijadili pia muswada wa bajeti wa mwaka wa fedha wa 2014/2015.
Wilaya hizo zitaungana na Manispaa za Kinondoni, Ilala na Temeke za jijini Dar Es Salaam linalokadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni 4.5.

No comments:

Post a Comment