MKAZI wa Shinyanga Julius John [30] ameuawa na wananchi
wilayani Kahama, kwa kupigwa na kisha kuchomwa moto baada ya kutuhumiwa kuiba
baiskeli na karanga zenye ujazo wa gunia moja.
Tukio hilo limetokea baada ya Julius kwenda nyumbani kwa
shangazi yake Justina John [48] katika kijiji cha Kasomela Kata ya Kinamapura
wilayani Kahama na kisha kufanya uhalifu huo.
Mlinzi wa amani kwenye Kata hiyo Clement Bilike ameeleza kuwa
baada ya Julius kuwa ugenini, shangazi yake alisafari huku akimuacha nyumbani
kwake na watoto.
Hata hivyo Julius alichukua baiskeli pamoja na gunia moja la
Karanga na kuanza kutoroka mnamo mida ya saa moja jioni hadi kijiji cha jirani
cha Ilemve ambapo baiskeli ilipata pancha.
Akiwa katika harakati za kutafuta namna za kuziba tairi ya
baiskeli hiyo alikamatwa na wananchi na kuanza kupigwa hadi kupoteza maisha na
baadaye kuchomwa moto na wananchi hao waliokusanyika baada ya kupigwa
yowe.
Polisi wilayani Kahama walifika kwenye tukio na kuruhusu
mabaki ya mwili wa marehemu Julius kuzikwa na kwamba uchunguzi juu ya tukio
hilo bado unaendelea
No comments:
Post a Comment